Loading...
title : MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI
link : MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI
MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.
Jenerali Mabeyo ametoa ushauri huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mabeyo amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya kuajiriwa .
“Vijana tunaowachukua JKT ni kwa ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili hata kijana akikosa nafasi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza kurudi kijijini akafanya vitu vya maendeleo, mimi nadhani watu wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT lazima aajiriwe, ipo haja ya kubadili mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo
“Jeshi linachukua vijana elfu ishirini kwa mafunzo, wanaochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama hawazidi vijana 2000 sasa hawa wengine 18,000 wanaenda wapi, kama mawazo yatakuwa ni kwenda JKT ili kuajiriwa hatutafanikiwa lakini kama watakwenda JKT kujifunza stadi za kazi kuwasaidia ili ziwasaidie kujiajiri na kubadili maisha yao tutafanikiwa sana” alisisitiza.
Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini kwake Juni 07, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa taarifa fupi ya mkoa kwa Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo(kulia) wakati alipomtembelea ofisini kwakeJuni 07, 2018 Mjini Bariadi na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka Mjini Bariadi, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi hao , Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo baada ya Mkuu huyo wa Majeshi kuzungumza na viongozi Mkoani humo Juni 07, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI
yaani makala yote MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mkuu-wa-majeshi-ahamasisha-vijana.html
0 Response to "MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA JKT KUPATA STADI ZA KAZI ZIWASAIDIE KUJIAJIRI"
Post a Comment