Loading...
title : MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU
link : MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU
MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo ametoa wito kwa wazazi kuwekeza katika elimu kwa watoto wao ili waweze kutimiza ndoto za maisha yao, badala ya kuwaoza wakiwa na umri mdogo.
Jenerali Mabeyo ametoa wito huo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya iliyofanyika Kijiji cha Masanza Kona kata ya Kiloleli Wilayani Busega, na kuhudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Vicent Naano marafiki wa mkuu wa majeshi kutoka Dar es Salaam , Wajenzi Enterprises ,wafanyabiashara wa Simiyu na waumini wa kanisa hilo .
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo pamoja na kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa amesema pamoja na jamii kushiriki katika ujenzi wa nyumba za ibada ,wazazi wanapaswa kutoa kipaumbele cha elimu kwa watoto badala ya kuwakatisha masomo hususani wa kike ili waolewe .
“Sasa hivi mmewekewa shule ya sekondari hapa na mimi nimeshiriki kujenga shule hii DC analijua hili, sasa wazee wangu mlioko hapa changamkieni elimu, watoto muwapeleke shule, waacheni wasome elimu ndiyo ufunguo wa maisha, wasiposoma hata mkiomba nafasi za kuingia jeshini hakuna nafasi” alisema Jenerali Mabeyo
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka akionesha sehemu ya fedha alizochangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akikabidhi sehemu ya fedha zilizochangwa na Kamti ya Ulinzi na Usalama na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiongoza Kwaya ya Kanisa Katoliki Parokia ya Ilumya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa ejngo la Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, (wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka akicheza pamoja na wanakwaya.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye kipaza sauti) akikabidhi sehemu ya fedha zilizochangwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la Kanisa Parokia ya Ilumya iliyoongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo katika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani humo.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbele ya jiwe la msingi la Ujenzi wa Kanisa Parokia ya Ilumya, baada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa ejngo la Kanisa, iliyofanyika Kijiji Cha Masanza kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, (katikati) Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU
yaani makala yote MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mkuu-wa-majeshi-atoa-wito-kwa-wazazi.html
0 Response to "MKUU WA MAJESHI ATOA WITO KWA WAZAZI KUWEKEZA KWENYE ELIMU"
Post a Comment