Loading...
title : MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA
link : MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA
MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii
MWANAMUZIKI wa nchini Nigeria Dapo Oyebanjo ‘D’banj’ amepoteza mtoto wake wa kiume wa pekee baada ya kutumbukia kwenye bwawa la kuogelea na kufariki dunia jana nchini Nigeria.
D’banj akiwa Los Angels kwenye tuzo za muziki za BET, msanii huyo aliweza kupewa taarifa za kifo za mtoto wake anayejulikana kwa jina la Daniel Oyebanjo III kuwa amezama na kufa maji.
Imeripotiwa kuwa mtoto huyo, Daniel Oyebanjo III, alizama kwenye bwawa la kuogelea (swimming pool) lililopo nyumbani kwa mwanamuziki huyo huko Ikoyi, jijini Lagos.
Hivyo D’banj aliripoti kifo cha mwanaye huyo wa mwaka mmoja kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kwa kuweka picha iliyotawaliwa na rangi nyeusi ikiambatana na ujumbe uliosomeka “Nyakati ngumu, lakini Mungu wangu ni mwaminifu, wakati wote na daima.”
Imethibitishwa kuwa mke wa mwanamuziki huyo, Lineo Didi alikuwa nyumbani wakati tukio hilo likitokea na haijajulikana kama kuna mtu aliyekuwa kwenye bwawa hilo huku.
Mapema wiki hii D’ banj katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ikiwa ni siku ya kina baba ‘Father’s Day’ akiwa anamvalisha mwanae pampers.
Hivyo makala MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA
yaani makala yote MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mtoto-pekee-wa-kiume-wa-dbanj-afariki.html
0 Response to "MTOTO PEKEE WA KIUME WA D'BANJ AFARIKI DUNIA NCHINI NIGERIA"
Post a Comment