Loading...

Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza

Loading...
Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza
link : Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza

soma pia


Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza

 




Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na Wahandisi (hawapo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). Kongamano hilo limefanyika leo jijini Dodoma.
 







  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema akitoa neno fupi la kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). Kongamano hilo limefanyika leo jijini Dodoma.

Mwamba wa habari
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka wahandisi nchini kujiongeza katika kutafuta fursa mbalimbali zikiwemo za ujasiriamali ili kujiongezea kipato.
Mwijage ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua Kongamano la Wahandisi zaidi ya 300 lililohusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (CRB). 
Waziri Mwijage amesema kuwa hakuna mtu anaezuiliwa kufanya kazi nyingine tofauti na aliyosomea hivyo hata Wahandisi wanaweza kufanya ujasiriamali wa aina yoyote.  
”Nawaomba Wahandisi kuchangamkia fursa pindi zinapotokea, mjitahidi mpate elimu ya ujasiriamali kwani Serikali itawatumia hata mkiwa katika Taasisi Binafsi", alisema Mwijage.
Aidha, Waziri Mwijage ametoa rai kwa Wahandisi kuungana kufanya kazi kwa pamoja bila ubaguzi ili kuwa pamoja katika ujenzi wa viwanda utakaopelekea nchi kuwa na uchumi wa kati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema amesema kuwa moja ya majukumu ya CRB ni kuhamasisha shughuli za uhandisi hasa katika shule na Vyuo Vikuu mbalimbali ili kwa miaka ijayo nchi ipate Wahandisi wengi watakaojenga miundombinu mbalimbali.
”Hadi kufikia leo, CRB imesajili jumla ya Wahandisi 21,746, tunatoa rai kwa Serikali kuendelea kutuamini kwa kutoa fursa zaidi kwa Wahandisi wa ndani kujenga miradi ya ujenzi inayoanzishwa nchini,” alisema Prof. Lema.
Bodi ya Usajili wa Wahandisi imeanzishwa kisheria mnamo Oktoba 10, 1968 kwa lengo la kusajili na kusimamia aina zote za Wahandisi na kukuza maendeleo ya uwezo wao kwa lengo la kulinda watumiaji wa huduma za ujenzi nchini.





Hivyo makala Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza

yaani makala yote Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/mwijage-awataka-wahandisi-kujiongeza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza"

Post a Comment

Loading...