Loading...
title : POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI
link : POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI
POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI
POLISI mkoani Morogoro inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu mwanamke aliyejifungua mtoto wakati akiwa njiani kupelekwa Kituo cha Afya Mang’ula, wilaya ya Kilombero mkoani humo mara baada ya kutolewa mahabusu ili kubaini kama kuna uzembe wowote umefanywa na watendaji ama askari na ikibainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Mugabo Wekwe ,alisema hayo jana katika taarifa yake kwa waandishi wa habari juu ya tukio la kujifungua mtoto njiani mwanamke Amina Rafael Mbunda (27) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa , Tarafa ya Mang’ula , wilayani Kilombero , mkoa wa Morogoro.
Alisema , Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio la mwanamke huyo aliyefikishwa katika kituo cha Polisi Mang’ula kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi kisha kujifungua akiwa njiani kuelekea katika Kituo cha Afya Mang’ula.
Alisema , Mei 31, mwaka huu ilifunguliwa kesi ya wizi wa samani mbalimbali zenye thamani ya Sh 1,040,000 katika kituo cha Polisi Mang’ula kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro zilizoibwa kwa vipindi tofauti katika karakana ya Joseph Mdee iliyopo maeneo ya Posta Mang’ula .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huyo alisema, baada ya tukio uchunguzi ulianza mara moja na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja alitwaje Ridhiwani Athuman na kukiri kuiba kisha kuwauzia watu mbalimbali akiwemo Abdallah Mohamed Mrisho (40) mkazi wa Kijiji cha Kiswanywa ,Tarafa ya Mang’ula.
Hivyo makala POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI
yaani makala yote POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/polisi-morogoro-watoa-ufafanuzi.html
0 Response to "POLISI MOROGORO WATOA UFAFANUZI MWANAMKE ALIYEJIFUNGUA NJIANI"
Post a Comment