Loading...

Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi

Loading...
Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi
link : Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi

soma pia


Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi

Na mwandishi wetu
VETERANI wa timu ya soka ya Uingereza ya Liverpool, Sami Hyypia amewataka vijana Watanzania kuongeza bidii katika kuhakikisha kwamba wanafikia hatua za juu za uchezaji soka hivyo kupata nafasi ya kucheza Ulaya.
Pia amesema ni matumaini yake kuwa mamlaka za utoaji leseni hazitawazuia vijana kwenda Ulaya kujaribu bahati zao.
Alisema hayo wakati wa kiliniki ya soka aliyoifanya kwa vijana wa Serengeti boys jana alipokuwa akishiriki nao katika mafunzo na mazoezi.
Alisema kwamba yeye hakuwa na kipaji kikubwa kuliko alivyoviona kwa vijana hao lakini ameweza kufikia hatua za juu kabisa za uchezaji wa soka kutokana na kujituma kwake.
Alisema amewaambia vijana kuangalia zaidi juhudi kwani kipaji pekee hakitoshi kumfanya mtu kuwa gwiji katika soko.
Alisema pamoja na mafundisho ya walimu ni kazi ya mchezaji mwenyewe kuona udhaifu wake uliopo na kuufanyia kazi ili aweze kuwa mwanasoka bora wa kutegemewa.
Akihojiwa mwanasoka huyo ambaye aliwika sana katika enzi zake alisema kwamba amefurahishwa na uchezaji wa timu hiyo hasa kwa pasi ndefu na kusema kwamba vijana wote wameonesha kuwa na vipaji vikubwa.
Alisema hata hivyo kwamba amewaambia wachezaji awali kuwa na kipaji pekee hakutoshi lakini ni lazima mtu binafsi kufanyakazi ya ziada kuondoa udhaifu wake ambao binadamu wengi wanakuwa nao ili kuwa mahiri katika uchezaji.
Sami ambaye yupo nchini kuangalia michuano ya kombe la benki ya Standard Charted  inayofanyika leo na kushirikisha timu 32 zinazowania kwenda Anfield kuona mechi za msimu mpya timu ya Liverpool  ndani ya EPL na kuzungumza na magwiji na kupata nafasi ya kunolewa, amesema siri kubwa ya mafanikio ni kujituma kwa mchezaji pamoja na kwamba anakipaji na walimu wazuri.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba akimtambulisha Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) kwa timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akizungumza na kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba (kulia) pamoja na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakimsikiliza kwa makini Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (hayupo pichani) wakati akiendesha kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kushoto) na Mshauri Mkuu wa Ufundi katika Programu za Soka la Vijana nchini, Kim Paulsen wakiangalia uzoefu wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.


 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akiendesha kliniki ya soka kwa vijana wa Serengeti Boys iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya gwiji huyo hapa nchini.
 Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) wakijinoa baada ya kupata mafunzo na mbinu mbalimbali wakati wa kliniki ya soka kwa vijana hao iliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia hapa nchini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi

yaani makala yote Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/sami-aridhishwa-na-vipaji-ataka-juhudi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Sami aridhishwa na vipaji ataka juhudi zaidi za kujituma kwa wachezaji binafsi"

Post a Comment

Loading...