Loading...

SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO

Loading...
SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO
link : SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO

soma pia


SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO

 Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Msajili wa Mashirika hayo Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau wanaofanya kazi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya Serikali kutoka katika Wizara, Taasisi na Mashirika ya Kiserikali jijini Dodoma ili kupata maoni yao juu ya Maboresho ya Sera ya Kitaifa ya NGOs ya mwaka 2001
 Mkurugenzi Msaidizi Usajili wa NGOs Bw. Leornard Baraka akielezea chimbuko la Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa wadau wanaofanya kazi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya Serikali kutoka katika Wizara, Taasisi na Mashirika ya Kiserikali jijini Dodoma ili kupata maoni yao juu ya Maboresho ya Sera ya Kitaifa ya NGOs ya mwaka 2001
 Baadhi ya wadau wanaofanya kazi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya Serikali kutoka katika Wizara, Taasisi na Mashirika ya Kiserikali na watendaji kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao kati yao kujadiliana na kupata maoni ya maboresho ya Sera ya Taifa ya NGOs kilichofanyika jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Anthony Ishengoma-WAMJW
Serikali imeyataka Mashirika  yote yasiyo kuwa za kiserikali ambayo yamejisajili tofauti na Sheria ya NGOs ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 kujisajili na sheria hiyo kabla Msajili wa NGOs nchini hajaanza kufanya uhakiki kwa kila shirika kuangalia kama usajili wao umezingatia matakwa ya Sheria husika.
Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini Bw. Marcel Katemba amesema hayo katika kikao chake na Maafisa Dawati wasimamizi kutoka Wizara , Mashirika na Taasisi za Serikali jijini Dodoma kujadili na kupitia Sera ya Taifa ya NGOs ili kutoa maoni yao kwa ajili ya marekebisho ya Sera hiyo inayofanyiwa mapitio mapya ili iweze kuendana mabadiliko mapya  ya kimaendeleo yaliyopo kwa sasa.
Amesema kabla ya Mwaka 2001 hapakuwepo Sheria Mahususi kwa ajili ya kusimamia Mashirika yasiyo ya Kiserikali hivyo kuyataka Mashirika yote ambayo hayajajisajili kwa Sheria ya NGOs ya Mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 kujisajili kabla Msajili hajafanya uhakiki na kupelekea hatua zinazoweza kuwafanya kusitisha huduma zao.
Aidha Bw. Katemba amesema kabla ya kutungwa kwa Sheria ya NGOs ya mwaka 2002 na baadaye kufanyiwa marekebisho mwaka 2005 Mashirika mengi yalijisajili na Sheria nyingine akitolea mfano wa Wizara ya Mambo ya Ndani na BRELA na kufanya kazi kama NGOs kwa mantiki  ameyataka Mashirika hayo kujisajili kwa Sheria ya NGOs inayompa Msajili mamlaka ya kusajili, kuratibu na kusimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kote nchini.
‘’Tunapitia upya Sera ya Taifa ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) ili iweze kuendena na mabadiliko mapya ya kimaendeleo ndio maana tunakutana na maafisa dawati la NGOs kutoka Wizara, Mashirka na Taasisi za Serikali ambazo tunaimani zinafanya kazi kwa karibu na Mashirika haya ili watoe maoni yatakayoweza kusaidia kuboresha Sera ya Taifa ya Mashirika haya.”Alisisitiza  Bw. Katemba.
Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi wa Mashrika ya Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii)  Bw. Leonard Baraka amesema uwepo Sheria na Taasisi nyingine zinazotawala mashirika yasiyo ya kiserikali bado ni changamoto katika kusimamia na  kutekeleza Sheria ya NGOs Nchini.
Aidha Bw. Baraka amesema uwepo wa Sheria na taasisi nyingi zinazofanya usajili na kusimamia baadhi ya mashirika hapa nchini ni changamoto kubwa inayopekea kulegalega kwa udhibiti wa mashirika haya jambo ambalo ni hatari kwa Taifa kwa kuwa baadhi ya Taasisi zinatumia fursa hiyo kuendeleza vitendo vya ualifu.

Wizara ya Afya inafanya maboresho ya Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001 pamoja na mambo mengine itaweka misingi itakayosaidia mashirika mengi kupunguza utegemezi wa fedha kutoka kwa wafadhili jambo ambalo litawezesha Mashirika kuweza kujitegemea kiuchumi tofauti na wakati huu ambapo wafadhili wakipunguza kufadhili Mashirika mengi yanakufa kwa kukosa fedha.


Hivyo makala SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO

yaani makala yote SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/sera-ya-taifa-ya-mashirika-yasiyo-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERA YA TAIFA YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KUFANYIWA MAPITIO"

Post a Comment

Loading...