Loading...

TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE

Loading...
TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE
link : TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE

soma pia


TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE

JIOGRAFIA/MAHALI LILIPO SOKO.

Soko la Katengele linapatikana katika vilele vya milima yenye msitu ujulikanao kama Iyondo - Mswima wenye miti ya asili na ile ya kupandwa ukizungukwa na Kata za Kalembo, Sange, Ibaba, Ngulugulu na Kufule.

Pia soko hili hupitiwa na Barabara ya Mkoa ya Ibungu - Ileje hadi KKK Wilayani Rungwe ikiligawa katikati na kuacha upande mmoja kuwa Kata ya Sange na upande mwingine Kata za Kafule na Sange.

HISTORIA YA SOKO:

Soko hili limekuwepo kwa muda mrefu likianzia kabla ya wakoloni, wakati wa ukoloni na baada ya Uhuru wa wetu mnamo 1961 hadi sasa.

Katengele awali palijulikana kama Katengele Bhalindu (yaani mabinti) ikielezwa kuwa ndipo palikutanisha vijana waliotaka kuoa au kuolewa kwa kabila la Wandali ambalo ni kubwa kwa Wilaya hii na maarufu kwa Mkoa wa Songwe na Mbeya kutokana na uchapaji kazi hususani zile za kutumia nguvu.

Kuhusu “Katengele Bhalindu” (yaani mabinti) hapa ndipo palipokuwa soko la awali pakiwa na msitu mdogo ambapo inasemekana kuwa mabinti wawili walipotea bila kupatikana katika mazingira ya kutatanisha kwa muda mrefu na imebaki kuwa simulizi inayoendelea kila linapotajwa neno katengele.

Awali lilikutanisha watu wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ileje na Wilaya za Mbozi, Rungwe na Kyela wakiuza bidhaa kwa fedha tasilimu pamoja na biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa. 

Kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa maarufu sana kwa biashara ya ng’ombe, bidhaa za asili pamoja na zile za viwandani likiwavutia hata raia wa Nchi jirani ya Malawi.

KUANZISHWA KWA MRADI WA SHAMBA LA MITI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wakala wa Misitu (TFS) imeamua kuanzisha Shamba la Miti la Iyondo - Mswima ukiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2015/2020 ibara ya 31 vifungu vya b,c,d,e na f kuhusiana sekta ya Maliasili.

Kwa mujibu wa Meneja wa Mradi wa Iyondo – Mswima Ndg. Deograsian Kavishe upandaji miti utaanza rasmi katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ikiwa baadhi ya kazi zilianza kutekelezwa na Mradi katika mwaka wa fedha 2017/2018.

Kuanzishwa kwa shamba hili la Katengele kunaifanya Tanzania kuwa na mashamba ya miti ya kupandwa 23 yakiwa yanapatikana katika Kanda mbalimbali kati ya hayo manne yapo katika hatua ya uanzishwaji likiwemo hilo la Iyondo – Mswima (Ileje).

Eneo la Mnada wa Katengele Wilayani Ileje mkoani Songwe unaotakiwa kuhamishwa ili kupisha Mradi wa Upandaji Miti.
Askari Jeshi USU (ambalo ni jina geni kwa wengi ) Deograsian Kavishe Meneja Mradiwa Upandaji Miti wa Iyondo-Mswima akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ileje.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mhe.Ubatizo Songa akiongoza Wahe. Madiwani na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje walipotembelea eneo la Mradiwa Upandaji Miti la Iyondo-Mswima.
Kitalu cha miti kilichopo Katengele-Ileje kikitarajiwa kubadilisha sura ya msitu wa Iyondo-Mswima wiyani Ileje
Eneo la Njiapanda ya Shule ya Msingi Mbangala panapotarajiwa kuhamishiwa Mnada wa Katengele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Ndugu Haji Mnasi (aliyesimama) akizungumza kwenye Baraza Maalum kuhusu Mnada wa Katengele.



Hivyo makala TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE

yaani makala yote TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/taarifa-kuhusu-kuhamisha-soko-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAARIFA KUHUSU KUHAMISHA SOKO LA KATENGELE - WILAYANI ILEJE"

Post a Comment

Loading...