Loading...
title : Taasisi ya Uhasibu nchini yaanzisha maombi kwa njia ya mtandao
link : Taasisi ya Uhasibu nchini yaanzisha maombi kwa njia ya mtandao
Taasisi ya Uhasibu nchini yaanzisha maombi kwa njia ya mtandao
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii
Taasisi ya Uhasibu Nchini (TIA) kimesema kuwa waombaji wa kozi mbalimbali katika chuo hicho wanaomba moja kwa moja kwa njia ya mtandao ikiwa ni kuwaondolea usumbufu kwenda vyuoni kwa kwa ajili ya udahili.
Akizungumza katika banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika moenesho ya 42 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Mhadhiri wa Taasisi hiyo Alex Marwa amesema kuwa watakaotembelea maonesho ya sabasaba watasaidiwa kufanya maombi ya kujiunga na chuo kwa njia ya Mtandao.
Amesema kuwa kwa waombaji wanaweza kuomba katika tovuti ya www.tia.ac.tz ambapo baada ya kuomba hapo atapata maelezo yote na kuunganishwa huduma nyingine za mahitaji ya chuo .
Amesema kuwa Chuo cha Uhasibu kinaendelea kutoa elimu bora kwa ajili ya maendeleo ya taifa kutokana na kozi zilizopo katika kila mwaka wa masomo .
Marwa amesema kuwa hakuna usumbufu wowote utaokaojitokeza katika maombi katika njia ya mtandao.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charle’s Kichere akitoa maelezo katika banda banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika moenesho ya 42 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akisaini kitabu cha wagene alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Taasisi ya Uhasibu katika moenesho ya 42 ya biashara ya kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Ofisa wa Idara ya Bajeti ya Serikali wa Wizara ya Fedha na Mipango, Boniface Kilindimo akitoa maelezo ya bajeti kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Charles Kichere akipata maelezo kuhusu Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma wa Bodi hiyo Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Shamim Mdee alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Hivyo makala Taasisi ya Uhasibu nchini yaanzisha maombi kwa njia ya mtandao
yaani makala yote Taasisi ya Uhasibu nchini yaanzisha maombi kwa njia ya mtandao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi ya Uhasibu nchini yaanzisha maombi kwa njia ya mtandao mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/taasisi-ya-uhasibu-nchini-yaanzisha.html
0 Response to "Taasisi ya Uhasibu nchini yaanzisha maombi kwa njia ya mtandao"
Post a Comment