Loading...
title : TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA
link : TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA
TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limezindua treni ya mizigo kuelekea nchini Uganda ikiwa imebeba shehena ya mzigo wa tani 2,400 wa Shirika la Chakula Duniani (WFP).
Kubebwa kwa shehena hiyo ya mizigo kwenye treni kumenusuru takribani dola 96,000 sawa na Sh.211,200,000 za gharama ya usafirishaji.
Treni hiyo iliyoanza safari leo imezinduliwa na Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji Focus Makoye Sahani na kueleza utekelezaji huo ni maagizo ya Rais wa Dkt John Magufuli kwa Wakurugenzi wa Shirika la Reli na mamlaka ya bandari kuhakikisha treni ya mizigo inafanya kazi akiwa katika ziara ya kikazi nchini Uganda.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sahani amesema kuwa treni hii ya mizigo ilisimama toka Agosti mwaka 2009 wakiwa chini ya mwekezaji ila kwa juhudi zilizofanywa na mamlaka ya bandari na shirika la Reli limefanikisha kurejea kwa usafiri huo kuelekea nchini Uganda.
Sahani amesema kuwa, kwa mara ya hii ya kwanza wamepata ofa ya tani 2,400 toka kwa WFP utakuwa ni kwa treni tatu pia wanashukuru kwani njia ya reli ni usafiri mzuri na wenye uhakika na wameweza kushirikiana na Shirika la Reli nchini Uganda na kufanikiwa kukarabati eneo la kilometa 9 kuelekea Kampala lililokuwa linasumbua.
"Tumeshirikiana na Shirika la Reli Uganda kufungua njia inayoelekea Kampala kwa kuwapatia vifaa vya kufungulia njia hiyo,"amesema Sahani.
Ameongeza amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuweza kupata vichwa vya treni vipya na vifaa vingine ambavyo vitaboresha huduma zao za usafirshaji kuanzia sasa.
Mkuu wa Usafirishaji wa WFP Muhamad Mabuyu amesema kuwa wameokoa dola 40 kwa kila tani ambapo thamani yake ni zaidi ya milioni 211 za kitanzania kama wangetumia usafiri wa njia ya barabara, na hiyo hela kwa sasa itatumika kununulia mahitaji mengine kwa ajili ya wahanga mbalimbali.
Mabuyu amesema, treni hiyo ya mizigo itatoka kuanzia katika hifadhi yao ya chakula bandarini Dar es Salaam na itafika moja kwa moja katika hifadhi yao ya nchini Uganda katika Jiji la Kampala.
"Tumeweza kutumia usafiri wa njia ya reli kwani ni rahisi na wenye uhakika kwakuwa mwaka 2017 tulisafirisha tani 16,000 kuelekea Mkoani Dodoma na haikupotea hata kiroba kimoja cha kilo 50,"amesema.
Mabuyu amesema,mbali na tani hizo zinazoelekea Kampala, kuna tani zingine 15,000 zinaanza kuingia kesho ambazo pia tutatumia usafiri wa njia ya reli kuzisafirisha na iwapo wangetumia magari ya tani 30 wangeingia gharama kubwa sana ya magari 500 ila watatumia treni 19 kufikisha mzigo huo .
WFP wamesifia huduma za TRC na kueleza yeye kama mdau wa usafirishaji anaupongeza uongozi wa TRC na Serikali kwa ujumla kwa kufanikisha huduma hiyo ya njia ya reli kurudi ikiwa ni baada ya miaka 10.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Focus Makoye Sahani akizindua treni ya mizigo na kuashiria kuanza kwa huduma hiyo baada ya kusimama kwa kipindi cha miaka 10.
Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Focus Makoye Sahani akizungumza na waandishi wa habari kabla kuzindua treni ya mzigo kuelekea nchini Uganda ikiwa ni baada ya miaka 10 toka kusitishwa kwa huduma hiyo ya usafirishaji.
Mkuu wa Usafirishaji wa Shirika la Chakula Duniani Nchini Tanzania (WFP) Muhamad Mabuyu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea ubora na ufanisi mzuri wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika ufanisi wa usafishaji mizigo wakati wa uzinduzi wa treni ya mizigo kuelekea Nchini Uganda.
Hivyo makala TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA
yaani makala yote TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/trc-yazindua-treni-ya-mizigoyabeba-tani.html
0 Response to "TRC YAZINDUA TRENI YA MIZIGO,YABEBA TANI 2,400 KUPELEKA NCHINI UGANDA"
Post a Comment