Loading...
title : WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT
link : WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT
WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT
JOSEPH MPANGALA,MTWARA
Wawakilishi wa Baraza la usafirishaji Korosho Kutoka Nchini India (CEPCI) wamefanya ziara Mkoani Mtwara na kukutana na wadau wa usimamizi,ununuzi na usafirishaji wa zao la Korosho kwa leno la kujadiliana namna bora ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa Biashara ya zao la Korosho kati ya nchi ya Tanzania na India.
Mkutano huo wa siku moja, umefanyika katika ofisi za Bodi ya Korosho TanzaniaCBT Mkoani Mtwara na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Vyama vya ushirika, wanunuzi wa Korosho, Mamlaka ya MapatoTanzania (TRA),pamoja na Mjumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini India.
Aidha Mkutano huo umejikita katika kujadili changamoto zinazojitokeza wakati wa kununua na kusafirisha Korosho kutoka Tanzania kwenda Nchini India ambazo ni pamoja na kuzingatia kwa ubora na uaminifu wa wasafirishaji. Mwenyekiti wa CEPCI Ktuoka Nchini India Raghavanpillai Bhoocles ameishukuru Bodi ya Korosho Tanzania kwa juhudi inazozifanya katika kusimamia Sekta ya Korosho Nchini,Na kushauri kufanyika kwa mikutano ya Mara kwa Mara kwa lengo la kuondoa changamoto chache zinazojitokeza.
Kwa upande wake Meneja wa udhibiti Ubora kutoka CBT Bw.Ray Mtangi amewahakikishia wawakilishi hao kutoka Nchni India kwamba tayari Serikali imeshaanza kushughulikia changamoto zilizojitokeza katika msimu wa Korosho uliopita wa 2017/2018 na kuahidi Kuzifanyia kazi
“Changamoto Chache zilizojitokeza katika Msimu Uliopita tayari Serikali imenza kuzifanyia kazi na tayari Tumejipanga ili kuhakikisha Changamoto Hizo Kutojitokeza tena katika Msimu Unaokuja”Amesema Mtangi

Meneja Uthibiti Ubora Kutoka Bodi ya Korosho CBT Ray Mtangi Akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya CBT na wajumbe wa Wakala wa Usafirishaji wa korosho kutoka nchini India uliofanyika Mkoani Mtwara.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Cashew Export Promotioncouncil of India {DEPCI} akizungumza katika mkutano wa pamoja na Bodi ya Korosho Jinsi ya Kuondokana na Changamoto katika Ununuzi na Usafirishaji wa Korosho.

Washiriki wa Mkutano wa wakijadili juu ya namna ya kuimarisha Uhusiano na kuboresha usafirishaji wa korosho kutoka Tanzania kwenda nchini India.
Hivyo makala WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT
yaani makala yote WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/wakala-wa-usafirishaji-watembelea-cbt.html
0 Response to "WAKALA WA USAFIRISHAJI WATEMBELEA CBT"
Post a Comment