Loading...
title : WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA
link : WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA
WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Elimu wahakikishe wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo ni wale waliovuka katika ngazi ya shule, kata, wilaya na mkoa, ambao wote ni wanafunzi halali wa shule na marufuku kuchezesha mamluki.
“Endapo itabainika yupo mchezaji aliyeletwa kushiriki michezo hii ambaye si mwanafunzi (yaani mamluki) naagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya wahusika kwa kuzingatia kanuni na sheria za mashindano haya,” amesisitiza.
Waziri Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Juni 9, 2018) wakati akifunguaMashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania yanayofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa mikoa na wilaya zote nchini wahakikishe kuwa masomo ya haiba, michezo na stadi za kazi yanafundishwa kikamilifu kwenye shule zote za msingi.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema somo la elimu ya michezo kwa Shule za Sekondari nalo lifundishwe kikamilifu na vyuo vya michezo kama Malya viendelee kuwaendeleza walimu wa michezo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipuliza kipenga kuamuru ipigwe penati wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Unguja wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Kagera wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wasita kushoto) wakitazama mechi ya mpira wa Kikapu kwa wanawake baada ya kufungua mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza na watano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. Pichani, Aisha Nasoro wa Dodoma (kulia) akimtoka Zurfa Maulid wa Singida.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wachezaji timu ya mpira wa Kikapu ya wanawake kutoka mkoa wa Singida wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kabla ya kufungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Bwiru ya jijini Mwanza wakionyesha halaiki kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Mashindano ya 39 ya UMISSETA na UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 9, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA
yaani makala yote WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/watakaochezesha-mamluki-umisseta.html
0 Response to "WATAKAOCHEZESHA MAMLUKI UMISSETA KUKIONA-WAZIRI MKUU MAJALIWA"
Post a Comment