Loading...
title : WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA
link : WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA
WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA
Na Linda Shebby, Chalinze
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) wamewakamata watu saba katika hifadhi ya Saadan ambao wamekutwa wakimiliki silaha ambazo walikuwa wakizitumia kufanyia uwindaji haramu katika hifadhi hiyo bila ya kuwa na kibali.
Huku wakituhumiwa kumuua myama mmoja adimu anayepatikana kwenye hifadhi hiyo ya Saadan pekee aliyemtaja kwa jina Pongwe
Akizungumza leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shanna amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Hadija Rashid ( 32 )mkazi wa Mkange amekamatwa na Magobore mawili, Amina Athumani (30) mkazi wa Gama amekamatwa na risasi tisa za Short Gun, Mohamed Athuman (65) mkazi wa Manda ambaye amekamatwa magobore mawili Yusuph Salum( 62) ,pamoja na Salum Ramadhan( 96)mkazi wa Manda amekamatwa na magobore mawili.
Kamanda Shanna amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni Athumani Abdully (26), Siwatu Bakari(40) na Mussa Abdully wote wakazi wa Manda na walipokamatwa kila mmoja alikiwa na gobore moja.
Kutokana na tukio hilo Kamanda Shanna ametoa siku moja kwa raia wanaomiliki silaha isivyo halali kuzisalimisha mara moja.
Katika tukio la pili Jeshi la Polisi mkoani hapa wamekamata gari lilikokuwa limeibiwa katika eneo la vigwaza mapema mwaka huu lenye namba za usajili T 265 BZC aina ya Mitsubish Canter tukio hilo lilitokea baada ya kundi la watu sita.
Huku mmoja wao akijifanya ni Mwalimu wa Shule ya sekondari Vigwaza akiwa na wenzake walimfuata dereva aitwaye Omari Nyange(39) na kumwambia kuwa wanataka kumkodi ili wakahamishe vyombo dereva huyo alikubaliana na watu hao na walipoanza safari ya kwenda eneo la Madafu walimbadilikia na kumkaba kisha kumpora gari hilo na yeye kumtupa nje.
Baada ya taarifa hizo kufika katika Jeshi la Polisi walianza upelelezi na Juni 6 mwaka huu wakalikamata katika Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro baada ya mwizi mmoja kukamatwa aliyetajwa kwa jina la Kasimu Nasoro(40) ambaye amekiri kuhusika na tukio hilo.
Amefafanua amekiri kuwa baada ya kuiba gari hilo walilibadilisha namba na kufunga namba za bandia ambazo ni T 525 ABM na kulisafitisha hadi Mangula.
Ambako walitengeneza kadi bandia na kwenda kuliuza kwa kiasi cha Sh. 8,000,000 kwa Florida Stanslaus mkazi wa Mang'ula Morogoro.
Katika tukio la tatu Jeshi la Polisi katika mzani wa Msata Wilaya ya Kipolisi Chalinze wamekamata madumu matupu yanayodaiwa kukamata gari aina ya fuso lililokuwa linaendeshwa na dereva likiwa limebeba vyuma chakavu ambavyo havikulipiwa ushuru wa serikali ambapo walitozwa faini kiasi cha Sh. milioni 2,000,000 na maofisa wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa kosa la kukwepa ushuru.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Jonathan Shanna akionyesha pembe ya mnyama ajulikanae kama pongo na silaha mbalimbali ambazo zimekamatwa katika misako inayoendelea.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Jonathan Shanna akionyesha gari lililokuwa limeibwa na kubadilishwa namba za usajili (bandia).
Hivyo makala WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA
yaani makala yote WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/06/watu-saba-wakamatwa-hifadhi-ya-saadan.html
0 Response to "WATU SABA WAKAMATWA HIFADHI YA SAADAN KWA TUHUMA ZA KUFANYA UWINDAJI HARAMU KWA KUTUMIA SILAHA"
Post a Comment