Loading...
title : CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa
link : CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa
CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8nEXhGZGgmo7LLo_U4R-2at7pUyNNdmi0-xBlvqP3dyWuHXUkGl1f2Z9ZHqwuUNtM-JdhgMZlBmNL3bGBQLM4cbqr6lSrut6FxELaE047ic2Q0IQrU34a_mEgHG8Ipe0_HoGowsEucPlO/s400/1.jpeg)
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Magdalena Sakaya ambaye ytuko upande wa Profesa Lipumba amesema chama hicho kitashiriki uchaguzi wa ubunge katika majimbo ya Buyungu, Jangombe na kwenye Kata 79.
Akizungumza jana Sakaya alisema chama hicho kimepokea barua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikielezwa kuwa majimbo na kata hizo, yapo wazi.
Alisema kutokana na mabadiliko yaliyofanyika NEC na katika vyombo vya Dola ni wazi kuwa wataibuka na ushindi katika chaguzi hizo
“Naomba ifahamike kuwa CUF ipo moja na uamuzi wa chama ni kushiriki uchaguzi, wanachama wasisikilize maneno ya watu ambao hawahusiki na chama," alisema Sakaya.
Alisema wapo wanaojitambulisha kuwa viongozi wa CUF wanasema hawatoshiriki, si kweli wamachama na wenye nia ya kutaka kugombea ubunge na udiwani wajitokeze.
"Uchaguzi wa ubunge jimbo la Kinondoni tulilalamikia utaratibu ulivyokuwa na namna NEC walivyokiuka. Ila kw amabadiliko yaliyofanyika sasa, naamini hali itakuwa nzuri,” alisema Sakaya.
Hivyo makala CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa
yaani makala yote CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/cuf-ya-lipumba-yasema-itashiriki.html
0 Response to "CUF Ya Lipumba Yasema Itashiriki Uchaguzi Mdogo Uliotangazwa"
Post a Comment