Loading...

DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi

Loading...
DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi
link : DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi

soma pia


DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mamlaka ya maji safi na maji taka (Dawasa) inatekeleza mradi Mkubwa wa upanuzi wa chanzo cha maji Chalinze ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mkoa wa pwani.

Mradi huo ambao kwa sasa uko katika hatua ya tatu  utahakikisha pia upatikanaji wa maji katika viwanda unakuwa wa uhakika.

Akiongea katika ziara  ya kukagua.. Maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji na upanuzi wa chanzo cha mtandao wa maji Chakinze, waziri wa maji na umwagiliaji, Profess Makame Mbarawa.amewahakikishia wawekezaji nchini kuwa jitahada kubwa zinafanywa kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa maji katika viwanda vyote kikiwemo cha Sayona.

Amesema, Dawasa kama sekta ya maji, watahakikisha wanatekeleza  azma ya kumaliza tatizo kubwa la maji hadi kwenye viwanda, kwani hakuna kiwanda kitakachoendelea bila ya kuwa na maji ya kutosha.

Naomba niwahakikishie watanzania wenzangu ambao wanania thabiti ya kujenga viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi wetu, sisi kama sekta ya maji tutahakikisha kwamba tunawapa nguvu zetu zote na kuwawekea miundombinu ya kisasa ili huduma ya maji iweze kuwafikia na waweze kufanya kazi zao za uzalishaji ili nchi yetu iweze kukua kufikia uchumi wa wakati 2025" amesema Mbarawa.

Aidha ameongeza, katika kutekeleza hilo tayari kuna mradi wa kupeleka maji kwenye kiwanda kikubwa cha Sayona ambao utahusisha kuuweka bomba la maji kutoka kwenye vyanzo vya maji mpaka kufikia kwenye kiwanda hicho, umbali wa kilometa 70 ujenzi ambao  utagarimu shilingi milioni 12

Wakati huohuo waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa Chalinze kuhakikisha unakamilika mwishoni mwa mwezi November mwaka huu. 

Amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua wakandarasi wanaochelewesha miradi kwani lengo la serikali ni kupeleka Huduma  bora ya maji kwa wananchi.

Mradi huo wa Chalinze utahusisha upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji wa Chalinze ambao chanzo chake ni mto Wami, lengo kubwa likiwa ni kuongeza uzalishaji kufikia Mita za ujazo 900 kwa saa kutoka mita za ujazo 500.

Mradi huo ambao mpaka utakapokamilika utagarimu USD 41,362023.43 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India kupitia Exim benki utahusisha pia ujenzi wa matanki 19,ulazaji wa mabomba ya ukubwa mbali mbali ya umbali wa kilometa 1022, ujenzi wa vizimba 351  vya kuchota maji katika vijiji na vitongoji vya Bagamoyo na Chalinze huku vizimba vingine vinatarajiwa kujengwa katika baadhi ya maeneo ya halmashauri za Handeni, Tanga na Ngerere mkoani Morogoro.

"Mradi huu ukikamilika wakazi wa pwani na Dar es Salaam watafadika na kusahau kabisa kero ya maji.


Hivyo makala DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi

yaani makala yote DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/dawasa-yatekeleza-miradi-ya-kuondoa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi"

Post a Comment

Loading...