Loading...
title : DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA
link : DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA
DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA
Na Hamza Temba-Kigoma
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla ameagiza wavamizi wote waliopo ndani ya Pori la Akiba Kigosi/Moyowosi na Hifadhi ya Msitu wa Makere mkoani Kigoma waondoke mara moja kupisha maeneo hayo yaendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa Sheria.
Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na uongozi wa mkoa wa Kigoma, ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Alisema taarifa za kiitelijensia zinaonyesha kuwa wengi wa wavamizi hao ambao wameanzisha makazi, kilimo na ufugaji ni raia kutoka nchi jirani ambao pia wamekuwa wakijihusisha na uharibifu wa mazingira na vitendo vya ujangili.
"Haivumiliki kwa kiongozi yeyote mzalendo kwa nchi yake ambaye anajua kabisa maeneo yetu yamewekwa akiba kwa ajili ya uhifadhi na tunawazuia hata wananchi raia kuyatumia alafu wanakuja raia wa nchi nyingine wanaachiwa wafanye wanavyotaka, hapana hili halikubaliki" alisisitiza Dk. Kigwangalla huku akiutaka uongozi wa Mkoa huo usaidie kusimamia Sheria na wavamizi hao waondoke mara moja.
Aidha, ametoa kipindi cha miezi mitatu kwa watu wote waliovamia maeneo ya kinga za hifadhi (bafa) ambayo ni mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na vijiji waondoke kwa hiari yao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Kigoma na Halmashauri husika pamoja na Wakala wa Huduma za Barabara TANROADS katika ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mkoa huo na maeneo mengine.
Alisema, Serikali ya awamu ya tano imepanga kufungua Sakiti mpya za utalii ikiwemo ya Kanda ya Magharibi ambayo inaujumuisha mkoa wa Kigoma, hivyo ni lazima miundombinu ya barabara ijengwe na kuimarishwa ipitike muda wote ili hifadhi hizo zitumike zaidi kibiashara na ziweze kuchangia ipasavyo kwenye pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa, Muongoza Watalii wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe, Iddi Kaluse kuhusu Maporomoko ya Maji ya Kakombe ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.
Baadhi ya Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipanda mlima kwa ajili ya kuwaona Sokwe Mtu katika Hifadhi ya Taifa Gombe alipotembelea hifadhi hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi mkoani Kigoma.
Msafara wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ukielekea Hifadhi ya Taifa Gombe kwa kutumia usafiri wa boti.

Hivyo makala DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA
yaani makala yote DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/dk-kigwangalla-aagiza-wavamizi-maeneo.html
0 Response to "DK. KIGWANGALLA AAGIZA WAVAMIZI MAENEO YA HIFADHI MKOANI KIGOMA WAHAME MARA MOJA"
Post a Comment