Loading...

DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17

Loading...
DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17
link : DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17

soma pia


DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17

Na Mathias Canal, Sengerema-Mwanza

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wametatua mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17.

Mgogoro huo umemalizika kwa maelewano ya pande zote mbili kuwa na kauli moja ambapo Mwenyekiti wa kijiji hicho amekubali kuketi meza moja na Uongozi wa chama hicho cha ushirika ili kukubaliana namna bora ya kuchochea Maendeleo katika kijiji na Taifa kwa ujumla badala ya kuendeleza mgogoro usiokuwa na maslahi kwa pande zote.

Alisisitiza umuhimu wa ushirika nchini ambapo aliwaeleza wananchi hao kutoendeleza vita ya kutokuwa na maelewano kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma shughuli za Maendeleo ya kijiji na Taifa kwa ujumla wake.

Pia, Dkt Tizeba ametangaza Kiama kwa maafisa ugani wanaokaa maofisini badala ya kuwasaidia wakulima kwenye hatua muhimu za uandaaji wa shamba na hatimaye wakati wa Kilimo.Katika mkutano huo Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe Dkt Angelina Mabula aliwataka wananchi hao kuwa na utamaduni wa kuketi pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili ili kuzitatua kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba, Naibu waziri wa ardhi, nyumba na  maendeleo ya makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Nyamatongo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baina ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Leo 8 Julai 2018.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza jambo wakati wa mkutano wa utatuzi wa mgogoro baada ya Chama Cha Ushirika Nyamatongo dhidi ya Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana uliodumu kwa miaka 17, Leo 8 Julai 2018.
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamatongo Ndg Itembwe Mnana (Kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha ushirika Nyamatongo Ndg Willium Elikana mara baada ya kuridhia mgogoro kumalizika.



Hivyo makala DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17

yaani makala yote DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/dkt-tizeba-na-dkt-mabula-wamaliza_8.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT TIZEBA NA DKT MABULA WAMALIZA MGOGORO WA ARDHI WA CHAMA CHA USHIRIKA ULIODUMU KWA MIAKA 17"

Post a Comment

Loading...