Loading...
title : JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP
link : JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP
JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP
Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi lipo mikononi kwa kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).
Wakili mwandamizi wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo leo Jumatatu Julai 23, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.
Mbali na Mrita, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017 ni mfanyabiashara Revocatus Muyela (40) ambapo wote wanakabiliwa na shtaka mmoja la mauaji ya dada yake Erasto Msuya, Aneth Msuya.
"Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na jalada la kesi kwa sasa lipo mikononi mwa DPP bado tunalifuatilia "amedai Mwita.
Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Simba amewataka upande wa mashtaka kulifuatilia jalada hilo ambalo mwanzoni walidai liko ofisini kwa DPP na sasa liko mikononi mwake.
Wakili wa utetezi Peter Kibatala alikubaliana na upande wa mashtaka na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine fupi.
Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 30, 2018 itakapotajwa tena.
Februari 23, 2017, washitakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa upya shtaka moja la mauaji.
Washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP
yaani makala yote JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/jalada-la-kesi-dhidi-ya-mke-wa-bilionea.html
0 Response to "JALADA LA KESI DHIDI YA MKE WA BILIONEA MSUYA LIKO MKONONI MWA DPP"
Post a Comment