Loading...
title : KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO
link : KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO
KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike amehitimisha ziara yake fupi mkoani Morogoro kwa kuongea na baadhi ya maafisa, askari na watumishi raia wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Morogoro na Gereza Kihonda.
Jenerali Kasike ametumia ziara hiyo ya kwanza tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Jeshi hilo Julai 13 mwaka huu kuwataka watendaji wote ndani ya Jeshi la Magereza kutambua alama za nyakati na kubadilika kabisa kimtazamo, kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kujisikia aibu kwa kuona Jeshi lao linatajwa kwa ubaya wa kushindwa kutimiza majukumu yake sawasawa.
Amewataka maafisa na askari wote kujiandaa kupokea mpango kazi wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa ambao hivi sasa unaandaliwa katika ngazi ya makao makuu ya Jeshi hilo.
Jenerali Kasike amewatolea wito viongozi wote ndani ya Jeshi la Magereza kuwa tayari kupokea maoni ya walio chini yao bila kujali vyeo vyao ili kuweza kufikia malengo tarajiwa.Aidha amesisitiza kuwa ni lazima watendaji wote kufuata maadaili kwakuwa suala la maadili ya kazi halihitaji raslimali ni mtu kubadilika tu.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike akikagua shamba la miwa la gereza Mbigiri, Morogoro lililopo chini ya mradi wa ubia kati ya Magereza na mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF. Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya tani elfu 30 za sukari kwa mwaka.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike (wa kwanza kushoto) akikagua baadhi ya matrekta na mitambo inayotumika katika kuandaa mashamba ya miwa ya gereza Mbigiri kwenye mradi wa ubia kati ya Magereza na mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF wa kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari. Jenerali Kasike ametembelea mradi huo leo Julai 27, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akitoa hotuba wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa zahanati ya gereza la Mahabusu Morogoro iliyofanyika leo tarehe 27 Julai, 2018.Kamishna Kasike alitumia hafla hiyo kuwakubusha na kuwasihi wageni waalikwa kuitikia wito wa serikali wa kupima afya zao mara kwa mara ikiwa ni njia mojawapo ya kupambana na ukimwi.
Mkuu wa Gereza la Mahabusu Morogoro Marakibu wa Magereza Zephania Neligwa akisoma risala kwa mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike katika hafla fupi ya uzinduzi wa zahanati ya gereza la Mahabusu Morogoro iliyofanyika leo tarehe 27 Julai, 2018. Mrakibu Neligwa amesema ujenzi wa zahanati hiyo pamoja na ununuzi wa vifaa vya tiba na dawa hadi inazinduliwa imegharimu zaidi ya shilingi 24.8 milioni.
Baadhi ya maafisa na askari wa Kingolwira Complex inayojumuisha Chuo cha Ufundi KPF, Gereza Mtego wa Simba, Gereza Mkono wa Mara na Gereza Kuu la Wanawake wakifuatilia kwa makini maelekezo ya kiutendaji kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipowatembelea kwa mara ya kwanza leo tarehe 27 Julai, 2018 mara baada ya kufanya uzinduzi wa Zahanati ya gereza la Mahabusu, Morogoro.
Hivyo makala KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO
yaani makala yote KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/kamishna-jenerali-kasike-afanya-ziara.html
0 Response to "KAMISHNA JENERALI KASIKE AFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI MOROGORO"
Post a Comment