Loading...
title : KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA
link : KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA
KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA
Na Mathias Canal-WK, Misenyi-Kagera
Uongozi wa kiwanda cha Sukari Kagera umeagizwa kuacha urasimu katika mfumo wa uuzaji wa Sukari wanayozalisha badala yake kuingiza mtaani kwa wingi Sukari kwa wananchi ili kuepuka kadhia ya upungufu wa huduma hiyo muhimu katika jamii.
Agizo hilo limetolewa na Mawaziri wa sekta ya Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na waziri wa sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wakati wakizungumza na uongozi wa kiwanda hicho Jana 11 Julai 2018 walipotembela kiwanda cha Sukari wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Juzi 10 Julai 2018.
Mawaziri hao kwa kauli moja wametoa siku 14 kwa kiwanda hicho kuongeza kasi ya uzalishaji kutoka uzalishaji wa Sukari kwa Tani 350-360 kwa siku ili kufikia walau Tani 450 mpaka 500 kwa siku kwani kufanya hivyo wataimalisha uwezo wa Sukari kupatikana kwa wingi kwa wananchi hivyo kuondoa usumbufu wa gharama katika ununuzi wa bidhaa hiyo.
Aidha, Mawaziri hao wametoa kalipio Kali kwa uongozi wa kiwanda hicho kwa kuwa na mawakala wachache wa usambazaji wa sukari jambo ambalo linapelekea ushindani wa kibiashara kuwa mchache mbinu inayopelekea Sukari kuuzwa kwa gharama isiyokuwa rafiki kwa watumiaji.
Walisema kuwa ndani ya muda mfupi uongozi wa kiwanda hicho unapaswa kutathmini upya namna ya kuongeza Uwekezaji ili kurahisisha huduma za wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 hatimaye kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ifikapo mwaka 2025.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba akikagua uzalishaji wa sukari wakati walipotembelea kiwanda cha Sukari Kagera wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Jana 10 Julai 2018, Jana 11 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wakikagua eneo linalo wakati walipotembelea kiwanda cha Sukari wakiwa kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani humo iliyoanza Jana 10 Julai 2018, Jana 11 Julai 2018.
Hivyo makala KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA
yaani makala yote KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/kiwanda-cha-sukari-kagera-chaagizwa_11.html
0 Response to "KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAAGIZWA KUACHA URASIMU KATIKA KUUZA SUKARI WANAYOZALISHA"
Post a Comment