Loading...
title : Lipuli yasajiri wachezaji wanne
link : Lipuli yasajiri wachezaji wanne
Lipuli yasajiri wachezaji wanne
Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii
TIMU ya soka ya Lipuli FC ya mkoani Iringa jana imekamilisha usajili wa wachezaji wake wapya wanne kutoka timu tofauti ili kuongeza nguvu kwenye msimu wa 2018/19.
Lipuli wameweza kuwapata nyota wawili waliowahi kukipiga klabu ya Simba pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Yanga , Paul John Nonga kutoka Mwadui FC ya Shinyanga aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Usajili umewahusisha beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, William Lucian ‘Gallas’ kutoka Ndanda FC ya Mtwara na mshambuliaji Miraj Madenge ‘Shevchenko’ kutoka Mwadui FC ambao wote kila mmoja amesaini mkataba wa mwaka mmoja pamoja na Issa Ally Rashid, mchezaji huru ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.
Gallas na Miraji waliwahi kukipiga katika klabu ya Simba kuanzia timu ya Vijana kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 na baadaye kuchwa mwaka 2014.
Lipuli iliyoanza vizuri msimu wake wa kwanza ndani ya ligi kuu vodacom wakiwa chini ya kocha Selemani Matola imedhamiria kufanya vizuri msimu kwa kufanya usajili utakaokuwa na tija na kuleta ushindani ndani ya ligi.
Beki William Lucian 'Gallas' akipokea kandarasi yake ya mwaka mmoja kuitumikia klabu ya Lipuli Fc ya Iringa.
Hivyo makala Lipuli yasajiri wachezaji wanne
yaani makala yote Lipuli yasajiri wachezaji wanne Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Lipuli yasajiri wachezaji wanne mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/lipuli-yasajiri-wachezaji-wanne.html
0 Response to "Lipuli yasajiri wachezaji wanne"
Post a Comment