Loading...
title : LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI
link : LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI
LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha linampeleka mmiliki wa Kampuni ya Lugumi, Said Lugumi ofisni kwake Dodoma Julai 31 mwaka huu.
Lugola ametoa maagizo hay oleo ofisni kwake jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa anamhitaji Lugumi ofisini kwake saa mbili asubuhi ya Julai 31 na kufafanua kuwa Lugumi alikuwa amepewa mkataba wa kufunga vifaa vya utambuzi wa alama za vidole baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kampuni yake.
“Najua Lugumi ni mtanzania mwenzetu na hivyo ninapomuhitaji najua atafika kwa wakati.Nitafurahi zaidi siku hiyo kama nikisikia mlango unagongwa na kasha baada ya kuufungua nikamuona Lugumi,”amesema Lugola.Alipoulizwa anamuitwa kwa ajili ya kitu gani akajibu ni vema ikafahamika kampuni yake ilikuwa imeingia mkataba na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, hivyo anataka kuzungumza naye.
MTAMBO WA KUTENGENEZA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Wakati huo huo Lugola amesema ili kukamilisha mchakato wa usajili na utoaji wa vitambulisho vya Taifa ambapo amemuagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamalaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) kuwalisha taarifa kamili kuhusu ununuzi wa mtambo wa kutengeneza kadi ghafi ambao bado haujaletwa.
“Katika hili namhitaji ofisni kwangu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA aje pamoja na mmiliki wa kampuni iliyopewa zabuni ya kuleta mtambo huo kwani alishapewa fedha dola milioni 14 ambazo ni sawa na Sh.bilioni 32.
“Hivyo siku hiyo nachohitaji ni kuuona mtambo au fedha zetu ambazo tutazipeleka benki tukiwa na ulinzi,”amesema.
Hivyo makala LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI
yaani makala yote LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/lugumi-aitwa-ofisini-kwa-lugola-saa.html
0 Response to "LUGUMI AITWA OFISINI KWA LUGOLA SAA MBILI ASUBUHI"
Post a Comment