Loading...
title : MADIWANI CHADEMA.CUF WAFIKISHWA MAHAKAMA WILAYA YA ILALA KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHWA
link : MADIWANI CHADEMA.CUF WAFIKISHWA MAHAKAMA WILAYA YA ILALA KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHWA
MADIWANI CHADEMA.CUF WAFIKISHWA MAHAKAMA WILAYA YA ILALA KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHWA
Madiwani wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mmoja wa Chama cha Wananchi CUF, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, wakikabiliwa na mashtaka mawali likiwamo la kushawishi rushwa ya Sh 25.
Washtakiwa hao ni Diwani kata ya Segerea, Edwin Kenan Mwakatobe (33) na Diwani wa kata Mchikichini Joseph John Ngowa (45) wote kutoka Chadena na Diwani wa kata ya Mnyamani kupitia CUF, Shukuru Abdallar Dege (42).Wakili wa Takukuru, Devotha Mihayo kutoka Takukuru amewasomea washtakiwa mashtaka yao leo Julai 30.2018 mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Mujaya.
Katika shtaka la kwanza mshtakiwa Mwakatobe anadaiwa tarehe isiyojulikana, Julai 2018 katika Wilaya ya Ilala akiwa Diwani wa kata ya Segerea na mjumbe wa kamati ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alishawishi rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya M/S M+M Architects Co. Ltd, Burhan Mvungi kama kichocheo cha kupendelewa katika tenda na LG/015/2017/2018/HQ/CS/07 Lot 03 ambayo nilikuwa chini ya muajiri wao.
Katika shtaka la pili inadaiwa kuwa madiwani hao, Mwakatobe, Ngowa na Dege Julai 24, 2018 katika baa ya Kwetu Pazuri iliyopo Tabata Wilaya ya Ilala, wote wakiwa wajumbe wa kamati ya fedha na utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walipokea rushwa ya Sh milioni 3 kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya M/S M+M Architects Co. Ltd, Burhan Mvungi kama kichocheo cha kupendelewa katika tenda na LG/015/2017/2018/HQ/CS/07 Lot 03 ambayo ilikuwa chini ya muajiri wao.
Hata hivyo, washtakiwa hao wamekana kutenda makosa hayo wako nje kwa dhamana.Kesi imeahirishwa hadi Agosti 13 , mwaka huu wa ajili ya kutajwa.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika, katika tarehe hiyo washtakiwa hao watasomewa Maelezo ya awali.
Hivyo makala MADIWANI CHADEMA.CUF WAFIKISHWA MAHAKAMA WILAYA YA ILALA KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHWA
yaani makala yote MADIWANI CHADEMA.CUF WAFIKISHWA MAHAKAMA WILAYA YA ILALA KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADIWANI CHADEMA.CUF WAFIKISHWA MAHAKAMA WILAYA YA ILALA KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/madiwani-chademacuf-wafikishwa-mahakama.html
0 Response to "MADIWANI CHADEMA.CUF WAFIKISHWA MAHAKAMA WILAYA YA ILALA KWA TUHUMA ZA KUSHAWISHI RUSHWA"
Post a Comment