Loading...
title : MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE
link : MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE
MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE
*Ni kutaka iendelee na kupanga kusoma usikilizwaji wa awali
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubaliana na ombi la upande wa Jamuhuri la kutaka kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali na uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe iendelee na kupanga kusoma usikilizwaji wa awali (PH)
Julai 31 mwaka 2018.
Pia Mahakama imeruhusu upande wa mashtaka kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo mara moja baada ya PH kusomwa. Hayo yamefikiwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri baada ya kesi hiyo kuja kwa kutajwa kutokana na kusimama kupisha maamuzi ya mahakama kuu.
Kutokana na maombi ya upande wa mashtaka yaliyokuwa yakiomba mahakama kuu kufanyia marejeo mwenendo wa kesi yao juu ya uamuzi wa mahakama ya Kisutu.Hata hivyo, Julai 20 mwaka 2018 Mahakama Kuu ilitoa uamuzi na kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa yalikuwa ni batili na kwamba yalikosa vigezo kisheria.
Mapema Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba Mahakama kulipangia shauri hilo tarehe ya kuwasomea washtakiwa PH kwa kuwa uamuzi wa mahakama kuu ulishatoka na ombi la utetezi kutupiliwa mbali. "Mheshimiwa, shauri hili leo limekuja kwa kutajwa kwa sababu tulikuwa tunasubiri maamuzi ya Mahakama Kuu, lakini kwa kuwa maamuzi yameishatolewa.
"Tunaomba tarehe ya kuja kuwasomea washtakiwa PH na kuanza kusikilizwa siku hiyo hiyo mfululizo kwa tarehe zitakazopangwa na mahakama," ameeleza Nchimbi,Hata hivyo, Wakili wa utetezi Nashon Nkungu kwa niaba Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya wanaowatetea washtakiwa amedai kuwa baada ya uamuzi ule wa Mahakama Kuu, washtakiwa wamefaili kusudio la kukata rufaa mahakama ya Rufani ambayo ilipokelewa Julai 20 mwaka 2018
Baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hivyo makala MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE
yaani makala yote MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mahakama-yakubali-ombi-la-upande-wa.html
0 Response to "MAHAKAMA YAKUBALI OMBI LA UPANDE WA JAMUHURI KESI YA VIGOGO CHADEMA IENDELEE"
Post a Comment