Loading...
title : Mbunge Malembeka azindua mafunzo ya chaki
link : Mbunge Malembeka azindua mafunzo ya chaki
Mbunge Malembeka azindua mafunzo ya chaki
Na Heri Shaban,Zanzibar
MBUNGE Angelina Malembeka amezindua mafunzo endelevu ya Kujifunza kutengeneza chaki kwa Jumuiya za Chama Mkoa wa Kasikazini Unguja.
Mafunzo hayo yarishirikisha Wajumbe wa umoja wa Wanawake UWT Mkoa,Makatibu na Wenyeviti wa Jumuiya ya Wazazi,Umoja wa Vijana ngazi ya wadi, Jimbo na Wilaya.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mbunge MALEMBEKA alisema mafunzo hayo yamekamilika wilaya ya kaskazini B bado kaskazini A.
"Mafunzo haya yamedhaminiwa na Ofisi yangu kabla mafunzo haya ya kuwajengea uwezo awali niliwapa Mashine za Chaki tatu kwa vikundi vyote vya Wanawake ili wazitumie kuzalisha chaki wakaziuze shuleni"alisema Malembeka.
Alisema jumuiya hizo amezikabidhi Mradi mkubwa wa Chaki wenye thamani ya shilingi milioni 7.5 ili wajishughulishe wasikae nyumbani Wawe Wajasiriamali huku wengine wakitafuta soko kwa maofisa elimu kwa ajili ya kuziuza.
Alisema mafunzo hayo yanaendelea ambayo yanaendeshwa na mkufunzi Sebastian Haule.
Kwa upande wake MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake UWT mkoa wa Kaskazini B Mariam Mwarami alimpongeza Mbunge MALEMBEKA kwa mafunzo hayo ya Kuwajengea uwezo ambapo aliahidi kuzitunza machine hizo na kuimalisha Mradi wa chaki.
Mariamu alisema watashirikiana na mbunge MALEMBEKA na kuendeleza kampeni ya kauli mbiu ya Mradi huo Mkoa wangu Kiwanda changu,Kaskazini Unguja.
Hivyo makala Mbunge Malembeka azindua mafunzo ya chaki
yaani makala yote Mbunge Malembeka azindua mafunzo ya chaki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mbunge Malembeka azindua mafunzo ya chaki mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mbunge-malembeka-azindua-mafunzo-ya.html
0 Response to "Mbunge Malembeka azindua mafunzo ya chaki"
Post a Comment