Loading...
title : MMILILI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO
link : MMILILI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO
MMILILI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO
Na Linda Shebby, Pwani
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mmiliki wa kiwanda cha kuchapisha nyaraka mbalimbali kinachofahamika kwa jina la Yukos Enterprises kilichopo katika eneo la Tondoroni Kata ya Kisarawe Mkoa wa Pwani aliyetajwa kwa jina la Magora Magira Masegese kwa tuhuma za kukihujumu kiwanda hicho kwa kukichoma moto katika majengo makubwa mawili yenye mitambo mbalimbali yaliyopo katika kiwandani hapo.
Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SSP Blasius Chatanda amesema kuwa Jeshi la Polisi pia linamshikilia Meneja wa Kiwanda hicho Elia Elson pamoja na walinzi wawili ambao ni Sai Kwilasa na Razi Kadilio kwa mahojiano zaidi na kuwa thamani ya mali iliyoungua bado haijafahamika hadi hivi sasa.
"Baada ya taarifa kutufikia tuliwasiliana na wenzetu wa zimamoto na kuweza kufanikiwa kufika kwa wakati na kuuzima moto huo kabla haujaenea kwenye majengo mengine yaliyopo kwenye kiwanda hicho" alisema Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SSP Chatanda.
Aidha Kalimu Kamand alisema kuwa baada ya jeshi hilo kufanya ukaguzi katika moja ya jengo ambalo moto uliwahi kuzimwa , walikuta majaba matano yaliyokuwa kwenye kona ya jengo hilo ndani yake kukiwa na mafuta aina ya petroli pamoja na karatasi rola lililokuwa limetandikwa kwenye korido za jengo hilo ambalo ndani yake kulikuwa na nyaraka mbalimbali ambazo zilikuwa zimemwagiwa mafuta ya petroli lakini hazikuweza kuungua.

Aidha Mrakibu Msaidizi huyo wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Pwani Happines Shirima amesema changamoto waliyokumbana nayo walipofika ni kutoka kwa mmiliki wa kiwanda hicho aliposhindwa kuwafungulia lango kuu kwa madai kuwa mtoto wake ndiye anayejua zilipofunguo gali iliyochangia wafikie uamuzi wa kuvunja mlango ili kuweza kuwaokoa baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwemo ndani ya kiwanda gicho wakati kikiwaka moto.
Hivyo makala MMILILI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO
yaani makala yote MMILILI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MMILILI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mmilili-wa-kiwanda-ashikiliwa-na-jeshi.html
0 Response to "MMILILI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO"
Post a Comment