Loading...
title : Mwigulu Nchemba Atumbuliwa, Kangi Lugola Achukua Nafasi Yake
link : Mwigulu Nchemba Atumbuliwa, Kangi Lugola Achukua Nafasi Yake
Mwigulu Nchemba Atumbuliwa, Kangi Lugola Achukua Nafasi Yake
Mwamba wa habari
Rais John Magufuli leo amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kama ifuatavyo:
Kangi Lugola, aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) sasa anakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo amechukua nafasi ya Mwigulu Nchemba.
Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo mchana huu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi.
Taarifa hiyo imesema kwamba nafasi ya Kangi Lugola inaenda kuchukuliwa na Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mussa Ramadhan Sima.
Aidha Rais amefanya uteuzi wa Naibu Waziri katika Wizara ya kilimo kutokana na umuhumu wa Wizara hiyo ambapo, Mbunge wa Morogoro Kusini Omary Mgumba ameteuliwa kushika nafasi hiyo.
Pamoja na hayo, katika mabadiliko hayo madogo, Rais Mgufuli amefanya Uhamisho Waziri Prof. Makame Mbarawa kutokea Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anaenda kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, huku aliyekuwa kwenye Wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe anaenda kuwa Waziri wa Uchukuzi.
Hata hivyo Balozi Kijazi amesema tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hao itatajwa hapo baadaye
Hivyo makala Mwigulu Nchemba Atumbuliwa, Kangi Lugola Achukua Nafasi Yake
yaani makala yote Mwigulu Nchemba Atumbuliwa, Kangi Lugola Achukua Nafasi Yake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mwigulu Nchemba Atumbuliwa, Kangi Lugola Achukua Nafasi Yake mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/mwigulu-nchemba-atumbuliwa-kangi-lugola.html
0 Response to "Mwigulu Nchemba Atumbuliwa, Kangi Lugola Achukua Nafasi Yake"
Post a Comment