Loading...
title : NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA
link : NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA
NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA
Na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgalu amefanya ziara katika Mkoa wa Mtwara na kubariki vijiji 167 kupata umeme katika awamu hii na hii ni katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)kwa kutimiza ahadi kwa wananchi.
Akizungumza na wakazi wa Mtwara katika kata ya Nanyamba, Mgalu ameeleza kuwa baada ya kusikia changamoto katika Halmashauri mpya ya Nanyamba hakuona sababu ya kutosimamia upelekaji wa huduma ya umeme Nanyamba.Na amemshukuru Mbunge na viongozi wa Mtwara kwa ushirikiano wao.
Mgalu amesema kuwa kama shirika linahudumia wateja wote bila kujali itikadi wala chama na wananchi kwao ni wateja na ahadi yao ya kuwaunganishia wateja kwa asilimia 50 kufikia 2020 lazima itimie.Aidha amelitaka Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) kuwahudumia wananchi wa Mtwara kwa kuzingatia mkoa huo unachangia uchumi wa Taifa kutokana na uzalishaji wa korosho.
Ameagiza shirika kuangalia na kuhakikisha huduma ya umeme inapatika.
Kuhusu gharama ya umeme Mgalu ameeleza kuwa bei ya kuunganisha umeme wa REA 27,000 pekee na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo katika kuhakikisha wanapata huduma ya umeme na amehaidi kuwatembelea tena mapema Oktoba ili kuweza kuona kama maagizo aliyotoa yamefanyiwa kazi.
Pia amehaidi kuongeza orodha ya vijiji katika mradi huo wa umeme hasa katika maeneo muhimu kama hospitali mrad ya maji ili shuguli ziweze kwenda sawa na wananchi kuweza kupata huduma hiyo.Kwa upende wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ameeleza kuwa umeme uliopo unatosheleza licha ya kuwepo kwa changamoto katika maeneo machache na mchakato bado unaendelea, na amewataka viongozi wa kada mbalimbali kwenda na kasi ya hapa kazi tuu.
Naye mkazi wa Mtwara Rajabu Mkaika amepongeza Serikali kwa kutoa huduma ya umeme bila kujali hali zao.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, na viongozi wengine wa Halmashauri ya Mtwara vijijini mkoa Mtwara wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA awamu ya Tatu (REAIII), kwenye kijiji cha Nalingu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa na baadhi ya vingozi wa mkoa wa Mtwara wakiwa katika picha ya pamoja.
Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nalingu mkoani Mtwara wakati wa ziara yake katika Mkoa huo ,ambapo vijiji 167 vinatarajiwa kupata umeme wa REAIII awamu ya tatu,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kutimiza ahadi kwa wananchi.Katika hatua nyingine Waziri Mgalu amewaomba wananchi hao kuhakikisha wanaitunza miundombinu ya Umeme
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Nalingu mkoani Mtwara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/naibu-waziri-wa-nishati-abariki-vijiji.html

0 Response to "NAIBU WAZIRI WA NISHATI ABARIKI VIJIJI 167 KUPATA UMEME MKOANI MTWARA"
Post a Comment