Loading...
title : NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA
link : NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA
NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA
Kwanza napenda kutumia fursa hii kuwapongeza vijana walioteuliwa kushika nafasi mbalimbali, tambueni Rais amewaamini na amewapa nafasi hizo ili mkawe chachu ya maendeleo katika maeneo yenu ya kazi ili kutekeleza ilani ya CCM na kutatua kero za wananchi hasa wanyonge.
Najua tangu taarifa ya uteuzi ilipotolewa mmepokea salamu nyingi za pongezi, nawasihi 'msilewe' kwani Rais Magufuli amekuwa akisema katika teuzi zake pongezi ni chache ila pole ndiyo nyingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, mefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa wizara, mikoa na wilaya mbalimbali. Ni uteuzi makini kwani Rais amezingatia sifa na mahitaji ya kiutendaji katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Tangu uteuzi huu ufanyike kumekua na maneno mengi mitandaoni ya kubeza na kejeli kwa baadhi ya wateule hawa wa Rais na huo ndiyo msingi wa andiko langu.
Wapo waliotumia maneno makali katika mitandao mbalimbali ya kijamii wakidai Rais Magufuli amewateua wapinzani waliokuwa wakimpinga wakati wa uchaguzi wa 2015 na kuwaacha vijana wa CCM waliohangaika usiku na mchana kuhakikisha kura zake zinatosha na CCM inashinda.Ukichunguza, ni watu hawahawa walipinga ununuzi wa ndege, wakawa wa kwanza kuipanda, wanapinga ujenzi wa reli ya kisasa, huku mataifa makubwa yakiona umuhimu wake, kiasi cha kumuahidi Rais wetu kumsaidia.
Ni hawa hawa walitangaza hatuwezi kujenga barabara za juu, lakini ndio watakuwa wakwanza kupita pale Tazara, wakienda kupanda Dreemliner pale Uwanja wa JK Nyerere.Watu hawa leo wameibuka kivingine wanajaribu kuuaminisha umma kwamba uteuzi uliofanywa na Rais unashaka ndani yake na hauna afya kwa wanaCCM. Hawa ni watu wa kupuuzwa. Nakupongeza Rais wangu Dk. John Magufuli kwa uamuzi wako wa kuwapotezea.
Eti wanadiriki kuwataja wateule hawa eti ni wapinzani kana kwamba hawakustahili kupewa nafasi hizo Patrobas Katambi, David Kafulila na Moses Machali. Katika hoja zao mitandaoni wengine wamediriki kusema uteuzi huu umeleta makundi mawili ndani ya chama kwamba eti umeibua vita kati ya CCM asilia wanaobaki watazamaji na CCM wahamiaji wanaopewa nafasi. Kauli kama hizi zinapaswa kupuuzwa kwani zinapandikiza chuki na kuchochea mpasuko ndani ya chama (CCM).
Kabla sijaendelea nitumie fursa hii kumkaribisha Patrobasi Katambi Dodoma, karibu mh DC tushirikiane kusukuma maendeleo katika jiji letu la Dodoma.Chama Cha Mapinduzi kimejengwa katika misingi ya umoja na ushirikiano unaohanikizwa na kaulimbiu ya Umoja Ni Ushindi. WanaCCM wamejengwa katika misingi hiyo na wanaamini hakuna kununa katika chama kwani kazi za kufanya zipo nyingi ndani na nje ya chama ni suala la muda tu! Hivyo hakuna sababu ya kununa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Hivyo makala NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA
yaani makala yote NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/nampongeza-rais-magufuli-kwa-uteuzi-huu.html
0 Response to "NAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UTEUZI HUU MAKINI-MKOTYA"
Post a Comment