Loading...
title : NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake
link : NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake
NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake
Na George Binagi, Morogoro
Naibu Waziri wa Madini Mhe.Doto Mashaka Biteko leo amekamata madini ya vito aina Rhodilite yanayokadiriwa kuwa tani saba katika nyumba ya mchimbaji na mfanyabiashara mmoja wa madini iliyopo Kata ya Magoweko wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Aliyekamatwa na madini hayo ambayo bado thamani yake haijafahamika ni Bw.James Mnene ambaye ni mchimbaji na mmiliki wa kampuni ya madini ya JJ.Mnene & Partiners inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya vito katika machimbo ya Rubeho wilayani Gairo.
Mfanyabishara huyo amejitetea kwamba alikuwa ametunza madini hayo nyumbani kwake huku akitafuta soko na kuomba asamehewe kwani yuko tayari kufuata taratibu za biashara ya madini.
Nyumba ya mfanyabiashara aliyekutwa amehifadhi madini ya vito wilayani Gairo
Madini hayo yakiwa nyumbani kwa mfanyabishara huyoMashine iliyokutwa nyumbani kwa mfanyabiashara huyo ambayo ilikuwa ikitumika kusagia mawe ya madini hayo
Naibu Waziri Biteko (kushoto) akizungumza baada ya kufika nyumbani kwa mfanyabishara huyo (katikati). Mfanyabiashara huyo ametiwa nguvuni kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria ambapo anatuhumiwa kukweka kulipa mapato ya serikali kwani tangu mwaka 2013 amelipa shilingi laki nne
Hivyo makala NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake
yaani makala yote NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/news-alert-mfanyabiashara-wilayani.html
0 Response to "NEWS ALERT: Mfanyabiashara wilayani Gairo mkoa wa morogoro akamatwa na madini nyumbani kwake"
Post a Comment