Loading...
title : OSHA YASISITIZA KUSIMAMIA VEMA MAJUKUMU YAKE YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
link : OSHA YASISITIZA KUSIMAMIA VEMA MAJUKUMU YAKE YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
OSHA YASISITIZA KUSIMAMIA VEMA MAJUKUMU YAKE YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi(OSHA) umesisitiza umuhimu wa kuendelea na majukumu yake kwa kuhakikisha afya na usalama wa wafanyakazi wote unasimamia kwa viwango vya usalama vilivyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Pia umesema unaendelea na kutao elimu katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuendelea kuwajengea uwelewa wafanyakazi kutambua umuhimu wa kufanya kazi katika mazingira yaliyo salama kiafya huku ukielezea namna ambavyo umekuwa ukitekeleza majukumu yake.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Ofisa Uhusiano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi(OSHA) Eliuter Mbilinyi wakati anatoa elimu kwa wananchi na kuelezea majukumu wanayoyafanya kwa mujibu wa sheria.Pia ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ya kukidhi matakwa ya Sheria ya Usalama na afya ya mwaka 2003 ambayo ametaja mambo kadhaa yanayotakiwa kufuatwa.Ametaja mambo hayo ni kusajili sehemu ya kazi na kupatiwa cheti, fanya tathimini ya vihatarishi vya kiusalama na kiafya katika eneo la kazi walau mara moja kwa mwaka.
Ameongeza pia kuandaa sera ya usalama na afya katika sehemu ya kazi, hakikisha kaguzi zote za kiusalama na afya mahali pa kazi zilizopo kwa mujibu wa sheria zinafanyika na hakikisha wafayakazi wako wanakuwa na afya njema kwa kuwapima afya zao.
Ameongeza pia hakikisha wafanyakazi wako wamepatiwa mafunzo ya huduma ya kwanza na kamati za afya na usalama."Tumekuwa tukifanya kazi katika maeneo mbalimbali ya kazi na pale ambapo tunabaini sheria hazifuatwi basi tunachukua hatu kwa mujibu wa sheria.Alipoulizwa iwapo kuna malalamiko yanayotolewa na waajiri kuhusu wafanyakazi wao kutozingatia usalama mahali pa kazi amejibu kabla ya malalamiko kufika kwao kumekuwepo na mabaraza sehemu za kazi.
"Moja ya jukumu la baraza hilo ni kushughulikia changamoto ambazo zinajitokeza na pale ambapo wataona ipo haja ya wao kutoa maelekezo basi wanafanya hivyo,"amefafanua.Kuhusu maonesho ya Biashara ya kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Mbilinyi amesema kuwa wanatumia maonesho hayo kuendelea kutoa elimu kwa wanachi kuhusu umuhimu wa kuzingatia usalama mahali pa kazi.
"Tunaendesha shughuli na majukumu yetu kwa kadri ya utaratibu na viwango vilivyowekwa. Kwa upande wa uwajibikaji ni kwamba tunawajibika kwa matokeo ya kazi zetu na kwa wadau wote katika hatua zote za kiutendaji,"amesema Mbilinyi wajati anaelezea majukumu yao kwa wananchi.
Hivyo makala OSHA YASISITIZA KUSIMAMIA VEMA MAJUKUMU YAKE YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
yaani makala yote OSHA YASISITIZA KUSIMAMIA VEMA MAJUKUMU YAKE YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala OSHA YASISITIZA KUSIMAMIA VEMA MAJUKUMU YAKE YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/osha-yasisitiza-kusimamia-vema-majukumu.html
0 Response to "OSHA YASISITIZA KUSIMAMIA VEMA MAJUKUMU YAKE YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI"
Post a Comment