Loading...
title : SERIKALI INA ANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHIMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO
link : SERIKALI INA ANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHIMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO
SERIKALI INA ANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHIMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO
NAIBU Waziri wa Madini ,Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) ,akizungumza wakati alipokwenda kutembelea machimbo ya chumvi na kuzungumza na uongozi wa machimbo ya chumvi ya kampuni ya uzalishaji chumvi ya H.J .Stanley Ltd,kijiji cha Kitame Bagamoyo Mkoani Pwani. wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majid Mwanga.
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO
NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, amesema serikali ina angalia namna ya kutumia chumvi inayozalishwa hapa nchini na kudhibiti uingizaji wa chumvi kutoka nje ya nchi. Pamoja na hilo ,serikali imeshaondoa kodi 11 ambazo zilikuwa kikwazo katika uzalishaji chumvi hivyo ni wakati muafaka wachimbaji wa mashamba ya chumvi wakanufaika na soko la ndani na nje ya nchi .
Akizungumza na uongozi wa machimbo ya chumvi ya kampuni ya uzalishaji chumvi ya H.J .Stanley Ltd,iliyopo kijiji cha Kitame ,Bagamoyo mkoani Pwani alisema, haiwezekani watanzania wakatumia zao hilo mtambuka nchi za jirani wakati wapo wazalishaji wengi nchini. Aliwapa changamoto wazalishaji hao ,kuhifadhi chumvi yao kwenye viwango bora ili kuendana na soko la ushindani.
"Eneo la Mashariki mwa nchi chumvi inayotumiwa inatoka nchi ya Kenya huku chumvi ya Uvinza Kigoma asilimia 30 inatumika eneo la Magharibi mwa Tanzania na asilimia 70 inauzwa nchi ya Congo" alifafanua Nyongo.
Nyongo aliwasisitiza ,kuhifadhi kwenye mifuko yenye uzito mbalimbali kuanzia robo kilo, kilo moja kwani kampuni hiyo inahifadhi mifuko ya kilo 50 ili kugusa matakwa ya kila mlaji. Naibu waziri huyo wa madini aliwaasa wachimbaji wakubwa ,kuwawezesha wachimbaji wadogo nao waweze kuingiza chumvi sokoni. Akizungumzia malalamiko aliyofikishiwa kuhusu kodi ambayo ni kero inayotozwa na TANAPA katika eneo hilo ,Nyongo alieleza amelichukua na atayafikisha katika mamlaka husika.
Awali mkurugenzi wa kampuni hiyo ,Richard Stanley alilalamikia kodi inayotozwa wakati wa kupita kwenye eneo la hifadhi ya Taifa (TANAPA)ambapo gari la tani 10 ,tani mbili zote zinaishia kulipa kodi hiyo.
Nae mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,alhaj Majid Mwanga alielezea juu ya suala la mpaka ambapo baada ya kupanuliwa kijiji hicho kilionekana kiko ndani ya hifadhi ya Saadani hivyo taratibu zinaendelea na muda si mrefu litatatuliwa.
"Lengo la serikali ni kuhakikisha migogoro inakwisha ,ila ninaomba muendelee kuheshimu mipaka ya hifadhi zetu ili kuishi kwa amani na kufanya shughuli zenu bila vikwazo " alisema alhaj Mwanga.
Alhaj Mwanga ,alisema mgogoro wa mpaka ulikuwepo Saadan ,Matipwili,Gongo,Kitame na Java ambapo kwa sasa tatizo hilo limeisha kwa eneo la Java na Saadan .
Kampuni hiyo imeajiri watu 27 na inazalisha tani kati ya 6,000 na 4,000 kwa mwaka na ilianza uzalishaji mwaka 1948.
Hivyo makala SERIKALI INA ANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHIMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO
yaani makala yote SERIKALI INA ANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHIMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI INA ANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHIMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/serikali-ina-angalia-uwezekano-wa.html
0 Response to "SERIKALI INA ANGALIA UWEZEKANO WA KUDHIBITI UINGIZWAJI WA CHIMVI KUTOKA NJE YA NCHI-NYONGO"
Post a Comment