Loading...
title : TAMBWE ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA.
link : TAMBWE ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA.
TAMBWE ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA.
Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ameibuka na kusema wanaumizwa na hali inayoendelea katika timu hiyo lakini haiwafanyi washindwe kupigana huku wakiwaomba mashabiki kuwa kitu kimoja kabla ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Yanga inatarajiwa kurudiana na Gor Mahia Jumapili ya wiki katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar baada ya kufungwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Championi, Tambwe alisema kwa sasa bado wanapita katika kipindi kigumu lakini hawezi kuwafanya washindwe kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano huku akiwaomba mashabiki wasichoke kuwasapoti.
“Tunajua matokeo hayakuwa mazuri kwetu katika mchezo wa kwanza kwa sababu hakuna ambaye alitegemea tutapoteza tena kwa idadi kubwa ya mabao lakini kwa kuwa wenzetu walitumia mapungufu yetu kupata matokeo.
“Nadhani huu ni wakati wa kuendelea kushikamana, mashabiki wetu hawapaswi kuendelea kukata tamaa japokuwa hatupo katika wakati mzuri kama ilivyokuwa zamani, hakuna ambaye ana furaha na kinachotokea kwa sababu wote tunataka kufikia mafanikio na ukiangalia tunaelekea kwenye ligi kwa nini wakate tamaa,” alisema Tambwe.
Hivyo makala TAMBWE ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA.
yaani makala yote TAMBWE ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAMBWE ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/tambwe-atoa-ya-moyoni-kuhusu-yanga.html
0 Response to "TAMBWE ATOA YA MOYONI KUHUSU YANGA."
Post a Comment