Loading...

Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile.

Loading...
Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile.
link : Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile.

soma pia


Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile.

Na Ofisi ya UNBoA, New York, Marekani. 

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CAG) Prof. Mussa Juma Assad leo tarehe 24 Julai, 2018 amekabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa nchi ya Chile. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York nchini Marekani baada ya Tanzania kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka sita (6) kuanzia Julai Mosi, 2012.   
Pamoja na kufanya makabidhiano hayo, CAG Prof. Assad pia amehudhuria Kikao cha Kawaida cha 72 cha Bodi hiyo na kuwasilisha jumla ya ripoti 13 za Ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN). Ripoti hizo 13 zilizowasilishwa na Prof. Assad  na kutiwa saini na wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya UN ni pamoja na Ukaguzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Wakimbizi wa Palestina na Mashariki (UNRWA), Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa UNRWA Wakazi (UNRWA – SPF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN – Women) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira  (UNEP). 
Ripoti nyingine ni za Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira ulio chini ya UNDPGEF, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira ulio chini ya Shirika UNEP-GEF, Mfuko wa Mikopo Midogo midogo ulio chini ya UNRWA - MD Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN Habitat), Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Mahakama ya Umoja wa Mataifa inashughulikia Mauaji ya kimbari ya Yugoslavia ya zamani (ICTY), pamoja na ripoti ya Mpango wa Kupunguza Shughuli za Mahakama za Kimataifa Zinazoshughulikia Mauaji ya Kimbari (MICT).    
Akizungumza baada ya kuwasilisha ripoti zake, Prof. Assad amesema kikao hicho ni cha mwisho kwa nchi ya Tanzania kuhudhuria kama Mjumbe wa Bodi ya UNBoA na kinatarajiwa kuhitimishwa kesho tarehe 25 Julai, 2018. Hata hivyo, Prof. Assad amefafanua kuwa Tanzania itaendelea  kuwa mjumbe mwangalizi ”Observer Member” kwenye Jopo la  Wakaguzi wa Nje wa  Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo baada ya kung’atuka kwenye nafasi ya Ujumbe wa Bodi hiyo.  
Prof. Assad amesema, katika kipindi cha miaka sita ya UNBoA, Tanzania haikuwa tu Mjumbe wa UNBoA bali pia ilipata fursa ya kuongoza Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa kipindi cha miaka miwili (2).  
2/2 
”Nimekuwa mwenyekiti wa UNBoA kwa miaka miwili mfululizo kuanzia  Januari Mosi, 2015 hadi 31 Desemba, 2016 ambapo nimekuwa na jukumu la kuwasilisha taarifa za UNBoA katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Nilitumia fursa hiyo kumshauri Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa niaba ya UNBoA njia bora ya kuimarisha mifumo ya udhibiti katika usimamizi wa fedha pamoja na kubadili muda wa uwasilishaji wa hesabu za Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yanatoa hesabu zake mwishoni mwa mwezi Aprili”, amesema CAG Prof. Assad.  
Tanzania inaingia katika historia ya dunia kuwa nchi ya kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na ya tatu (3) Barani Afrika kuteuliwa mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA) tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo mwaka 1946.  Nchi nyingine za Afrika ambazo zimewahi kuwa wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa ni Ghana na Afrika ya Kusini tu.   
Tanzania imekuwa mjumbe wa Bodi hiyo kuanzia  Julai Mosi, 2012 hadi tarehe 30 Juni, 2018 baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa mjumbe wa Bodi hiyo mnamo tarehe 11 Novemba, 2011,  kwenye Kikao cha 58 cha Baraza hilo. Tanzania ilishirikiana na wajumbe wengine wa Bodi kutoka nchi za Uingereza, China, Ujerumani na India kwa vipindi tofauti.  

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad (katikati ya waliokaa) akitia saini ripoti za Ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani. Wengine ni  Mwenyekiti wa UNBoA na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi (wa kwanza kulia) pamoja na Rais wa Taasisi Kuu ya Ukaguzi Ujerumani Bw. Kay Sceller (wa kwanza kulia) kwa pamoja wakitia saini Ripoti 28 za Ukaguzi wa Mashirika na Mifuko ya Umoja wa Mataifa kwenye kikao hicho
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad (wa kwanza kushoto) akimkabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Chile wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani. Prof. Assad amekabidhi nafasi hii baada ya Tanzania kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka sita (6) kuanzia Julai mosi, 2012.  Mwingine ni Mwenyekiti wa UNBoA na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi akishuhudia makabidhiano hayo.
 Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mada wakati wa Kikao cha 72 cha Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) na  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa India Bw. Rajiv Mehrishi (katikati) akimshukuru na kumpongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Mussa Assad (wa kwanza kushoto) baada ya Tanzania kumaliza muda wake wa kipindi cha miaka sita (6) kuanzia Julai mosi, 2012 cha Ujumbe wa UNBoA na kukabidhi nafasi yake kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Chile. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Kikao cha 72 cha UNBoA  kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani.
Ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye picha ya pamoja nje ya lango la Ukumbi wa Mkutano baada ya kuhudhuria hafla ya kutia saini ripoti za Ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kukabidhi nafasi yake ya Ujumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Chile baada ya Kikao cha 72 cha UNBoA kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 24 Julai, 2018 jijini New York nchini Marekani.



Hivyo makala Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile.

yaani makala yote Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/tanzania-yapongezwa-kwa-kazi-nzuri.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Tanzania Yapongezwa Kwa Kazi Nzuri Ukaguzi Umoja wa Mataifa. Yamaliza kazi Rasmi na Kukabidhi Nchi ya Chile."

Post a Comment

Loading...