Loading...

TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake

Loading...
TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake
link : TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake

soma pia


TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake

Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya Kuifadhi Mafuta ya Tanzania (TIPER) imekabidhi kwa Rais John Pombe Magufuli gawio la sh bilioni 3 ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 6 kwa mwaka 2017 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Kampuni ya ADDAX-ORYX GROUP ya nchini Uswiss. 

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo Prof Abdulkarim Mruma alisema kiasi hicho ni ongezeko kutoka kiwango cha sh bilioni 1 kwenye miaka ya mwisho ya 2000 na wastani wa karibu sh bilioni 2 katika kipindi cha kati ya 2010-2013. “Uongozi wa Kampuni unaona fahari kubwa kuweza kusimamia uendeshaji na kuweza kukuza gawio kwa wanahisa wake.’’ Alisema. 

Akizungumzia mpango wa upokeaji wa Mafuta kwenye ghala moja ambapo kampuni hiyo inatarajia kuwa kituo pekee cha upokeaji wa mafuta yote yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar Es Salaam, Prof Mruma alisema manufaa yanayoyotarajiwa kupatikana kutokana na mpango huo yameshajadiliwana kupokelewa vyema na wadau wote. 

“ Faida za mpango huu zipo wazi ambazo ni pamoja na udhibiti bora wa kiwango cha mafuta kinachoingia nchini, kupunguza upotevu na wizi wa mafuta, kuzifanya gharama za ucheleweshaji wa meli zinazolipwa sasa kwa wamiliki wa nje wa meIi kuwa mapato ya serikali.’’ alitaja 

Alisema IIi kufanikisha mradi huu, Bodi ya Wakurugenzi ya TIPER imepitisha mpango mahususi wa uwekezaji wa zaidi ya Dolla za Marekani milioni ishirini na mbili (USD 22m) ndani ya kipindi cha 2018 mpaka 2019. 
Rais John Pombe Magufuli (katikati) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh bilioni tatu kutoka kwa Mwenyeki wa Bodi ya kampuni ya Kuifadhi Mafuta ya Tanzania (TIPER) Prof Abdulkarim Mruma ikiwa ni sehemu ya gawio la sh bilioni 6 ambalo kampuni hiyo imetoa kwa wanahisa wake ambao ni serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na pamoja na Kampuni ya ADDAX-ORYX GROUP ya nchini Uswiss. Wengine ni pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Phillip Mpango (kushoto kwake). 



Hivyo makala TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake

yaani makala yote TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/tiper-yakabidhi-gawio-la-bilioni-6-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TIPER yakabidhi gawio la bilioni 6 kwa wanahisa wake"

Post a Comment

Loading...