Loading...

TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA

Loading...
TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA
link : TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA

soma pia


TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA



Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia kupeleka timu ya wataalam wa fani mbalimbali 167 katika nchi tano tofauti kwa lengo la kujifunza namna ya kusimamia uendeshaji wa treni ya kisasa itakayotumia umeme.

Hatua hiyo inakuja wakati Serikali ikiendelea na ujenzi wa reli ya kisasa maarufu Standard Gauge Rail(SGR) ambapo treni yake itasafiri kwa kasi ya umbali wa kilometa 160 kwa saa.Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TRC Masanja Kadogosa amesema timu ya wataalamu hao itaondoka wakati wowote kuanzia sasa.

Amefafanua watalaam hao watatoka katika kada mbalimbali zikiwamo za watalaam wa mawasiliano, umeme, madaraja, usafirishaji, mafundi na madereva.Ametaja nchi ambazo wameingia nazo makubaliano ya kuwafundisha wataalam hao ni Korea Kusini, Uturuki, Ethiopia, China na India." Tumeamua hivyo kutokana na kwamba tunahitaji kuwajengea uwezo watalaam wetu kutoka kwa nchi ambazo zenyewe zina uzoefu wa uendeshaji wa reli ya aina hii. Watalaam hao wataondoka muda wowote kutoka sasa,amesema.

Amefafanua kwa wanaokwenda nchini Uturuki waliamua kusubiri kidogo kutokana na mchakato wa uchaguzi wa nchi hiyo.Akizungumza ujenzi wa reli hiyo amesema utaambana na ujenzi wa karakana za kisasa ambazo zitaenda sambamba na matumizi na teknolojia mpya inayotumia umeme tofauti na karakana zilizopo.Ameongeza ujenzi wa reli hiyo utamalizika kwa wakati kama ilivyopangwa kwani unaendelea kwa kasi na ufanisi mkubwa na tayari mkandarasi ameahidi kuongeza vifaa na watalaam.

Amesema ujenzi wa nguzo katika eneo la kutoka Stesheni ya Dar es Slaam mpaka Stesheni ya Ilala unaendelea vizuri ambao ni asilimia 30 ya ujenzi wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Stesheni ya Pugu.Akizungumzia mikakati ya TRC amesema licha ya ujenzi wa reli ya kisasa pia wanaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya reli katika maeneo mbalimbali.

Amesema lengo ni kuongeza uwezo wa shirika katika kutoa huduma ya usafirishaji wa mizigo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TRC Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na waandishi wa habari katika banda la shirika hilo kwenye viwanja vya maonesho vya Sabasaba leo wakati akizungumzia maen deleo ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya SGR kutoka Dar-Moro- Dodoma na ukarabati wa Reli ya Kati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Bw. Masanja Kadogosa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Baadhi ya wageni kutoka mataifa kadhaa ya nje waliofika kwenye banda la TRC wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa TRC.


Hivyo makala TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA

yaani makala yote TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/trc-kupeleka-watalaam-167-kujifunza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRC KUPELEKA WATALAAM 167 KUJIFUNZA UENDESHAJI WA TRENI YA KISASA"

Post a Comment

Loading...