Loading...
title : WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER
link : WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER
WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER
*Washauri inunuliwe na ndege ya mizigo ili kusafirisha bidhaa za Tanzania
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAFANYABIASHARA wa nchini Oman wamesema wamefurahishwa na hatua ya Rais Dk.John Magufuli kununua ndege ya Dreamliner huku wakishauri inunuliwe na ndege ya mizigo itakayotumika kusafirisha bidhaa za Tanzania na nchi yao.
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara kati ya Tanzania na Oman Sheikh Saud Al Rawadhi amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa baraza ambapo wafanyabiashara wa nchi hizo mbili wamekutana kujadii fursa za kibiashara kati ya nchi hizo.
Sheikh Al Rawadhi ametumia nafasi hiyo kueleza wameona Dreamliner imetua nchini Tanzania na kwamba wafanyabiashara wa Oman wanampongeza Rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hiyo.
“Tunampongeza Rais Magufuli kwa kununuzi Dreamliner .Ni hatua nzuri katika kuimarisha sekta ya anga nchini.Wafanyabishara wa Oman tunaomba ipatikane na ndege ya mizigo itakayotumika kusafirisha bidhaa za Tanzania kwenda Oman,”amesema Sheikh Al Rawahi.
Kwa upande wa mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa baraza la kibiashara Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi amewataka wafanyabiashara nchini Tanzania kuchangamkia fursa ya kibiashara kwa kuuza bidhaa zao nchini Oman.
Naibu Katibu MKuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki,Balozi Ramadhani Mwinyi akizungumza mapema jana jijini Dar kwenye mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Oman na Wafanyabiashara wa Tanzania , wakijumuika kwa pamoja kwenye kongamano la biashara, kwa madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.
Balozi Mwinyi alisema kongamano hilo ni muhimu kwa Wafanyabiashara hasa kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawajalitumia vyema soko lililopo nchini oman, kuuza bidhaa zao kutokana na nchi hiyo kuhitaji bidhaa nyingi kutoka nje kunakosababishwa na hali yake ya uzalishaji nchini OMAN.
Mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara nchini Oman,Saud Al Rawadhi akizungumza mapema jana jijini Dar kwenye mkutano wa pamoja kati ya ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Nchini Oman na Wafanyabiashara wa Tanzania , wakijumuika kwa pamoja kwenye kongamano la biashara, kwa madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.
Mwenyekiti huyo amewataka Watanzania amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kufanyabiashara OMAN huku akisisitiza kuwa baraza lake litatowa msaada wa kila aina ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanafanya biashara na Oman bila vikwazo vyovyote.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika Mashariki na Kati-Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Suleiman Saleh akizungumza mbele ya wageni waalikwa wa Kongamano la Kibiashara kati ya Tanzania na Oman,liliofayika mapema jana jijini Dar Es Salaam.Ambapo kongamano hilo lilikuwa na madhumuni ya kupeana fursa za bishara zilizomo ndani ya nchi hizo mbili.
Sehemu ya Meza Kuu ikifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo wakati wa majadiliano ya Kibiashara Baina ya Tanzania na Oman kwenye kongamano la pamoja lililofanyika jana jijini Dar
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Oman wakipeana ushauri na kubadilishana ujuzi wa kibiashara
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wawakilishi kuhusiana na fursa zilizopo katika nchi zao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER
yaani makala yote WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wafanyabiashara-wa-oman-wampongeza-rais.html
0 Response to "WAFANYABIASHARA WA OMAN WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUNUNUA DREAMLINER"
Post a Comment