Loading...

WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200

Loading...
WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200
link : WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200

soma pia


WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200

WAFANYABIASHARA wa Soko la Mabibo, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wamemuomba Rais John Magufuli kuingilia kati na kuzuia mpango wa manispaa kuwaondoa wafanyabiashara hao na kuwahamishia Soko la Simu 2,000.

Akizungumza na waandishi wa habari Mmoja wa Wafanyabiashara George Mligo alisema, viongozi wa Manispaa ya Ubungo wamewataka wahame katika soko hilo ambalo linauza mazao na matunda mbalimbali.Mligo alisema wanamuomba Rais Magufuli aingilie kati sakata hilo ili kupata ufumbuzi. Mligo alisema, awali waliambiwa watapelekwa soko la Makuburi lakini baadae walipewa taarifa kuwa eneo hilo lipo karibu na mto hivyo wanapaswa kuhamishiwa Soko la Simu 2,000 ambalo ni dogo.

Alisema katika soko la Mabibo kuna zaidi ya wafanyabiashara 4,000 ambao wanauza viazi, ndizi, nyanya, vitunguu, matunda na mbogamboga.“Kilio kikubwa tulichonacho wafanyabiashara wa soko la Mabibo, Serikali imeshindwa kututafutia soko lenye hadhi ya Kimataifa kama walivyoahidi na kinyume chake wanataka kutupeleka soko la Simu 2000 ambalo haliwezi kupokea zaidi ya watu 1,500 huku sisi hapa tupo zaidi ya 4,000,” alisema.

Mligo alisema, mchango wa soko hilo kwa mwezi ni zaidi ya Sh. Milioni 120 hivyo kitendo cha manispaa kuwaondoa katika eneo hilo kitapoteza fedha nyingi.Akizungumzia kadhia hiyo Mfanyabiashara Swadaka Magesa alisema, hawapo tayari kuhama katika soko hilo kwani hoja za Serikali hazina mashiko kwa sasa hasa kwa kukosa eneo ambalo linaweza kuwatosha.Magesa alisema iwapo watapatiwa eneo lenye sifa ya kupokea wafanyabiashara zaidi ya 4,000 na magari 130 kwa wakati mmoja watahama kwani wanaamini watafanya biashara kwa uhuru.“Kusema kweli Simu 2,000 sio sehemu sahihi ya sisi kuhamia kwani hata vitengo viwili haviwezi kuingia kwani eneo ni dogo hadi tunawaita tumeandika barua hadi kwa Rais Magufuli kumuomba aje kuona hali hii ili atusaidie,” alisema.

Akizungumzia sakata hilo Meya wa Manispaa hiyo Boniface Jacob, alisema, sio kwamba wanawahamisha ila ni mwenye eneo ambaye ni Kiwanda cha Urafiki kuhitaji eneo lake.“Sio kwamba tunawahamisha, Urafiki wanataka eneo lao ambalo wanalimiliki kisheria sasa sisi tufanyeje.“Eneo ambalo tunaweza kuwahamishia ni Simu 2,000 kwani manispaa haina maeneo, lakini naomba umtafute Mkurugenzi ataeleza kila kitu,” alisema.Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo simu yake iliita bila kupokelewa na baadae alituma ujumbe kuwa hawezi kuzungumza.
Mmoja wa Wafanyabiashara wa Soko la Mabibo George Mligo akieleza kwa hisia juu ya kuchukizwa na zoezi la wao kutolewa katika soko hilo 



Hivyo makala WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200

yaani makala yote WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wafanyabishara-mabibo-waligomea-soko-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAFANYABISHARA MABIBO WALIGOMEA SOKO LA SIMU 200"

Post a Comment

Loading...