Loading...
title : WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII.
link : WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII.
WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII.
Watendaji na Watumishi wa Serikali katika jiji la Arusha wametakiwa kushirikiana,kupendana na kufanya kazi kwa bidii ili kulinda mafanikio ya kimaendeleo yaliyofikiwa na jiji hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Arusha na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ambaye sasa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya Ofisi jijini hapo.
Akizungumza na Watumishi na Watendaji wa jiji hilo Dkt. Kihamia amewataka wafanye kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta mgawanyiko miongoni mwao. Amesema katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mkurugenzi wa jiji hilo aliwaunganisha watumishi wote akiweka msisitizo katika bidii, nidhamu ya kazi na matumizi mazuri ya rasilimali na fedha Serikali hali iliyolifanya jiji hilo kupata Hati Safi ya Matumizi ya fedha za Serikali.
“Watumishi Wenzangu mimi nimekaa katika jiji hili kwa muda wa miaka 2, nafurahi kuwa nawaacha mkiwa na morali ya kufanya kazi na muendelee kufanya kazi kwa bidii, mzidi kupendana ili kazi mnazozifanya zifanikiwe kwa manufaa ya jiji ” Amesisitiza Dkt. Kihamia. Ameongeza kuwa ili jiji hilo liendelee kupiga hatua zaidi za Kimaendeleo, watendaji na wakuu wa Idara wana wajibu wa kufanya kazi kwa pamoja, kuaminiana na kuepuka kufanya vitendo vya dhuruma na uonevu wa aina yoyote kwa watumishi wa kada mbalimbali walio chini yao.
Hivyo makala WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII.
yaani makala yote WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/watumishi-jiji-la-arusha-watakiwa.html
0 Response to "WATUMISHI JIJI LA ARUSHA WATAKIWA KUDUMISHA UPENDO NA KUFANYA KAZI KWA BIDII."
Post a Comment