Loading...
title : WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI
link : WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI
WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI
VICTOR MASANGU, KISARAWE
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo amewataka waratibu wa elimu kata kuachana kabisa na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na uzembe na badala yake watimize majukumu yao ipasasavyo bila ya kutegeana kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi pikipiki 17 kwa waratibu wa elimu kata katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuweza kuwawezesha vizuri usafiri kwa ajili ya kuweza kusimamia na kuboresha sekta ya elimu katika maeneo mbali mbali hususn vijijini.
Pia Jafo amewaagiza maafisa elimu wote kuhakikisha wanaweka mipango endelevu ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi, ambapo pia ametoa onyo kali kwa waratibu hao ambao watazitumia pikipiki hizo kwa kufanyia shughuli nyingine kwa maslahi yao binasfi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe Hamisi Dikupatile amemshukuru Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kuamua kutoa pikipiki hizo 17 ambazo zitaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa waratibu wa elimu kata ambao hapo awali walikuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na kuwepo kwa changamoto ya kusafiri umbari mrefu kwenda katika vituo vyao vya kazi.
Naye Afisa elimu wa Wilaya ya Kisarawe Shomari Bane aliahidi kulisimamia kwa hali na mali suala la usimamizi kwa waratbu wote wa kata kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu kwa kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule ya msingi pamoja na sekondari na kuondokana na changamoto ya kushuka kwa elimu.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoa wa Pwani kwa kipindi cha muda mrefu imekuwa ikibabiliwa na changamoto kubwa ya kufanya vibaya katika sekta ya elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kupekekea kuzindua kampeni maalumu kwa ajili kuweza kutokomeza divisheni ziro.
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo akiwasha moja ya pikipiki kati ya 17 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya kuwapatia waratibu elimu wa kata katika halmashauri ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu na kuongeza ufaulu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Raisi Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo akiendesha moja ya pikipiki kati ya 17 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano kwa ajili ya kuwapatia waratibu elimu wa kata katika halmashauri ya Kisarawe,Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweza kuongeza ufanisi katika sekta ya elimu na kuongeza ufaulu.
Waziri wan chi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Seleman Jafo akimkabidhi funguo mmoja wa waratibu wa elimu kata wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, ambao wamepatiwa pikipiki 17 kwa ajili ya kusimamia sekta ya elimu.(NA VICTOR MASANGU)
Hivyo makala WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI
yaani makala yote WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/waziri-jafo-akabidhi-pikipiki-17-kwa.html
0 Response to "WAZIRI JAFO AKABIDHI PIKIPIKI 17 KWA WARATIBU WA ELIMU KATA HALMASHAURI WILAYA YA KISARAWE MKOA WA PWANI"
Post a Comment