Loading...

WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO

Loading...
WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO
link : WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO

soma pia


WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea tabia ya kutowajibika miongoni mwa watumishi kwa kisingizio cha mgawanyo wa madaraka.

Ametoa onyo hilo jana (Jumamosi, Julai 7, 2018) wakati akizungumza na wanaushirika na mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini humo.


Amesema kuna maafisa ushirika ambao hawataki kuwajibika kwa sababu wameajiriwa TAMISEMI na wengine wako chini ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika."Afisa Ushirika wa Wilaya yuko mkoani ambako ni chini ya TAMISEMI, Mrajis Msaidizi wa Mkoa yuko Wizarani. Serikali ni moja, kwa hiyo wote bado mnawajibika kwa Mrajis Msaidizi wa Mkoa," alisema.

Aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri (DED) wasiwapangie kazi nyingine zilizo nje na taaluma yao maafisa ushirika wa wilaya na wahakikishe wanatoa taarifa kwenye vikao vya Halmashauri zao.

"Msimpe kazi ya kufundisha Afisa Ushirika kwa sababu hakuna mtu mwingine. Afisa Ushirika aachwe afanye kazi ya ushirika na atoe taarifa kwenye vikao vyenu. Madiwani mnapokutana kwenye Baraza, mpeni nafasi Afisa Ushirika aeleze maendeleo ya ushirika yakoje katika wilaya yenu."

Alisema changamoto nyingine zinazoikabili sekta ya ushirika ni wizi na ubadhirifu miongoni mwa watendaji wa vyama vya ushirika waliopewa dhamana ya kuvisimamia na kuviendesha vyama hivyo.Alisema changamoto nyingine ni ukosefu wa elimu ya kutosha ya ushirika miongoni mwa wanachama, viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika; kuporomoka kwa imani ya ushirika miongoni mwa jamii na kwa baadhi ya wanachama kutokana na vyama vya ushirika kushindwa kukidhi mahitaji ya wanachama wake.



Hivyo makala WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO

yaani makala yote WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-akemea-maafisa-ushirika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU AKEMEA MAAFISA USHIRIKA WENYE VISINGIZIO"

Post a Comment

Loading...