Loading...
title : WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA
link : WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA
WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea mahusiano mabaya baina ya watumishi wa wilaya ya Kahama na kusema wanapaswa kubadilika mara moja.
Ametoa onyo hilo leo (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
“Hali ya mahusiano hapa Kahama ni mbaya kuliko Kishapu na Shinyanga. Mnachapa kazi vizuri lakini tatizo kubwa kila mmoja anaenda kivyake, hakuna anayemsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri wala Mkuu wake wa idara,” amesema.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani humo, amewaeleza watumishi na viongozi hao kwamba Serikali haitavumilia kuona watumishi wa aina hiyo wanaendelea kufanya kazi.
“Serikali haitavumilia kuona watumishi wakifanya mambo ya hovyo. Kahama ni wilaya yenye majaribu na Shinyanga nayo ni wilaya yenye majaribu makubwa. Kwa hiyo watumishi inabidi muwe makini, kuweni waangalifu msije mkaingia kichwakichwa kwenye majaribu haya.”
“Migogoro niliyoisikia ambayo iko hapa ni kwa sababu ninyi mmeingia kwenye biashara na kutake sides. Hapa Kahama, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya hamuelewani, Mkurugenzi na wakuu wa idara hamuelewani, wakuu wa idara na wasaidizi wao nao pia hawaelewani,” alisema.“Napenda kusisitiza kwamba ninyio ni viongozi wa umma, kwa hiyo ni lazima mzingatie itifaki za kiuongozi, mzingatie mahusiano mema mahali pa kazi. Hatupendi viongozi muwe chanzo cha matatizo hapa Kahama,” aliwaasa.
Hivyo makala WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA
yaani makala yote WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-akemea-mahusiano-mabaya-ya.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AKEMEA MAHUSIANO MABAYA YA WATUMISHI KAHAMA"
Post a Comment