Loading...

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni.

Loading...
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni.
link : Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni.

soma pia


Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kufungua Sherehe za Kijadi za Mwaka Mpya Mwaka Kogwa, mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.

Waziri Mkuu wa Jamuhuru ya Muungano Tanzania.Mhe.Kassim Majaliwa amesema ipo haja ya viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya siasa kuhuburi umuhimu wa umoja na mshikamo sambamba na kuzikumbusha jamii zao kuezi mila na tamaduni walizorisi kutoka kwa wazazi wao.

Waziri Majaliwa aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Makunduchi Mkoa wa kusini Unguja kufuatia maadhimisho ya sherehe maalumu za mwaka kogwa ambazo hufanyika kila mwaka.

Amesema tabia ya kuhifadhi mila ma desturi huwanafanya wananchi kuendelea kuishi katika mazingira bora ya ujirani mwema.

Alieleza kuwa licha ya kuwa Tanzania ina makabila yasiopungua 120 lakini ni jambo la faraja sana hadi leo hii wananchi wa Makunduchi wanaendelea kudumisha mila walizorisi kwa wazazi wao tangu karne ya 18.

Pamoja na hayo aliwataka wazazi wa eneo hilo kuhakikisha utamaduni huo unaenziwa na kuedelezwa vizazi hadi vizazi.

"Cha kufurahisha zaidi ni kwamba nimeona sherehe hizi pia zinakuza utalii leo kuna wageni wamekuja kutoka Ujerumani na mataifa mengine ya ulaya hivyo muna kila sababu ya kuendeleza na kulikuaza"aliongeza Majaliwa.

Kwa upande wake mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Mhe.Haroun Ali Suleiman alimtaka Waziri mkuu kutumia sherehe hio kama sehemu ya kuendeleza umoja baina ya watu wa makunduchi na Tanzania bara.

Alieleza kuwa anaamini sherehe hizo zitaibua fursa mpya ya mashirkiano baina ya pande mbili za Jamuhuri ya Muungano licha ya kuwa wananchi hao wamekua na udugu wa miaka mingi.

Nae Naibu Waziri wa Vijana,Utamaduni Michezo Zanzibar.Mhe.Lulu Msham Abdalla alisema shehe hio pia ni fursa ambayo Zanzibar inaweza kuitumia kutangaza utalii wake.

Aidha alieleza kuwa kupitia tamasha hilo linaongeza kipato kwa wajasiriamali wa eneo hilo.

Aidha alisema wizara yake imejipanga kuhakikisha matamasha mbali mbali yanaboreshwa kwa lengo la kuikuza na kuitunza Zanzibar ndani na nje ha Nchi.


Hivyo makala Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni.

yaani makala yote Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/waziri-mkuu-wa-tanzania-mhe-kassim.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Awataka Wananchi Kudumisha Utamaduni."

Post a Comment

Loading...