Loading...
title : WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI
link : WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI
WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuhukumu muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni mbili au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja baada ya kupatikana na hati. a katika kesi ya kukutwa na kutumia dawa za kulevya
Hata hivyo, Mahakama imewaachia huru wafanyakazi wake Wema, Matrida Abbas na Angelina Msigwa aliokuwa akishtakiwa nacho baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao
Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.
Akisoma hukumu hiyo leo Hakimu Mkuu Simba amesema, upande wa Mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa, mshtakiwa Wema alitenda kosa la kutumia na kukutwa na dawa za kulevya.
Kabla ya kusomwa kwa Hukumu hiyo leo Julai 20 mwaka 2018, mashahidi upande wa mashtaka kupitia Wakili wake, Constantine Kakula waliwasilisha mashahidi 5 ambao wameweza kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka kuwa mshtakiwa Wema ametenda kosa.
Kwa upande wa washtakiwa walitoa utetezi wao wakiongozwa na Wakili Albert Msando na walipomaliza walifunga ushahidi wao na kufunga kesi yao.Pande zote ziliwasilisha hoja za majumuisho za mwisho na hatimaye kesi ikapangiwa tarehe ya hukumu .
Huku watuhumiwa akijitetea wenyewe.
Wema na wafanyakazi wake hao walikuwa wakishtakiwa na kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha madawa ya kulevya chini ya kifungu cha sheria namba 17 (1)(b) cha sheria inayodhibiti matumizi ya dawa za kulevya.
Walidaiwa kutenda kosa hilo Tarehe 4 February mwaka jana huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio
Pichani kulia Wema Sepetu akiwa na Mama yake wakiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya
Wa pili kulia Wema Sepetu akiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.Wema Sepetu aliambatana na Mama yake pamoja na Ndugu,jamaa na marafiki zake.
Wa pili kulia Wema Sepetu akiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akisubiri kusomewa hukumu yake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi ya dawa za kulevya.Wema Sepetu aliambatana na Mama yake pamoja na Ndugu,jamaa na marafiki zake.
Hivyo makala WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI
yaani makala yote WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wema-sepetu-ahukumiwa-mwaka-mmoja-jela.html
0 Response to "WEMA SEPETU AHUKUMIWA MWAKA MMOJA JELA AU KULIPA FAINI SH.MILION MBILI"
Post a Comment