Loading...
title : *WILAYA YA UBUNGO KUBORESHA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA KIMARA NDANI YA MIEZI MITANO*
link : *WILAYA YA UBUNGO KUBORESHA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA KIMARA NDANI YA MIEZI MITANO*
*WILAYA YA UBUNGO KUBORESHA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA KIMARA NDANI YA MIEZI MITANO*
Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa wilaya ya Ubungo mh. Kisare Makori wakati akikifunga kituo cha Afya Kimara kilichopo kata ya Saranga kwa muda wa miezi mitano.
Mkuu wa wilaya wilaya alisema uamuzi huo ni kwa faida ya wananchi wa kimara na maeneo ya jirani kwa ujumla. *"Baada ya kituo hiki kufungwa na maboresho kufanyika wananchi wa hapa ndio watakaofaidika"* Alisema Makori.
Aliongeza kuwa maboresho hayo ni katika kutekeleza ilani ya chama tawala katika sekta ya Afya ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Pia kaimu Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dr. Mariam Malliwah alitoa taarifa fupi ya Kituo cha Afya Kimara kata ya Saranga kwa mgeni Rasmi mh. Mkuu wa wilaya ya Ubungo ndg. Kisare Makori.
Kaimu Mganga mkuu alisema kuwa mbali na huduma mbali mbali zitolewazo na kituo hicho, kumekuwa na changamoto kadha wa kadha.
Baadhi ya changamoto hizo ni uhaba wa vyumba vya madaktari, maabara kubwa, wodi za kulaza wazazi wanaokuja kujifungua, jengo la upasuaji na huduma za X-ray.
*"Kutokana na changamoto hizi ofisi ya rais TAMISEMI kwa kushirikiana na uongozi wa Manispaa walikichagua kituo hiki kuwa miongoni mwa vituo vilivyopata fedha za ukarabati toka ofisi ya rais TAMISEMI"* Aliongeza Dr. Malliwah
Aidha tangu tarehe 08/05/2018 Manispaa ya Ubungo imepokea kiasi cha *Tshs. Milioni 500* na tayari ipo kwenye akaunti ya kituo. Vile vile Manispaa imetenga *Tshs milioni 200* kutokana na mapato yake ya ndani ili kujenga gorofa.
Kaimu Mganga Mkuu alimweleza mgeni rasmi kuwa kwa sababu ya ufinyu wa eneo lililopo kituo cha afya, imepelekea kupata idhini ya kujenga Majengo mapya na kubomoa majengo yote ili kupisha ujenzi mpya.
Baada ya maelezo hayo ya Kaimu Mganga Mkuu, mgeni rasmi alitangaza kituo hicho cha Afya Kimara kata ya Saranga kufungwa kwa muda wa miezi mitano.
*"Natangaza kituo hiki kitafungwa kuanzia tarehe 25 mwezi huu wa saba yaani leo hadi tarehe 25 mwezi wa 12, ina maana kitafungwa kwa muda wa miezi mitano"* Alisema mgeni rasmi.
*"Hata baada ya kituo hicho kufungwa kuna baadhi ya huduma bado zitaendelea kutolewa katika eneo la jirani la kanisa la parokia ya kimara ambalo baba Paroko kwa kushirikiana na kamati tendaji ya Parokia wamekubali kutupatia. Huduma hizo ni Afya ya baba, mama na mtoto ambazo ni kupima watoto uzito, chanjo na wamama wajawazito"* Aliongeza Dr. Malliwah
Kwa niaba ya wananchi ndg. Augustino Mabula ambaye ni mkazi wa kimara aliushukuru uongozi wa Manispaa kwa kuamua kupanua kituo hicho cha Afya. Alisema kituo hicho kimekuwa kikihudumia watu wengi pamoja na kuwa na miundombinu michache hivyo upanuzi huo utakuwa ni ukombozi kwa wananchi wa kimara na maeneo ya jirani.
*IMETOLEWA NA*
*KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO*
*MANISPAA YA UBUNGO*
Hivyo makala *WILAYA YA UBUNGO KUBORESHA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA KIMARA NDANI YA MIEZI MITANO*
yaani makala yote *WILAYA YA UBUNGO KUBORESHA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA KIMARA NDANI YA MIEZI MITANO* Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala *WILAYA YA UBUNGO KUBORESHA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA KIMARA NDANI YA MIEZI MITANO* mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/07/wilaya-ya-ubungo-kuboresha-huduma.html
0 Response to "*WILAYA YA UBUNGO KUBORESHA HUDUMA KATIKA KITUO CHA AFYA KIMARA NDANI YA MIEZI MITANO*"
Post a Comment