Loading...

AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR.

Loading...
AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR.
link : AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR.

soma pia


AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR.


Wanafunzi wa Shule ya Seminari Al Mutanzir Islamic Wakizungumzia mashindano ya mdahalo leo jijini Dar wa Salaam, kutoka Julia ni Husseina Nurbhai akiwa na mwezake Saloha Aboud

Mkuu wa Shule ya Al Mustazir Beuben Kimani akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Mimamizi wa mdahalo Shule ya Al Mutanzir Islamic Gertrude Mtenga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam kuhusu mashindano ya mdahalo.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaaam.
Zaidi ya wanafunzi 200 kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wamekutana nchini Tanzania kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya mdahalo 'Mwalimu Nyerere' yanayofanyika katika Shule ya Seminari ya Al Mustazir Nslamic jijini Dar es Salaam.

Mdahalo huo umeandaliwa na Shule ya Al Mutanzir Islamic yenye lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi wa kujiamini, kuchanganua mada mbalimbali, kujenga hoja na kuzitetea pamoja na kufanya vizuri katika mithiani yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Shule ya Al Mustazir Beuben Kimani, amesema kuwa  madahalo huo utafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.

Amesema kuwa katika mdahalo wanafunzi kutoka Shule mbalimbali  watashindana na Agosti I2 mwaka huu washindi watapewa zawadi.

Kimani ameeleza kuwa kuna wanafunzi zaidi ya nusu ya washiriki wametoka nchini mbalimbali Kenya, Zimbabwe, Zambia pamoja na Namibia.

"Kwa hapa Tanzania miongoni mwa shule zinazoshiriki ni Al Muntazir Islamic, Sabani Robert, Fedha Boys, Fedha Girls, Aghakhani, Tusime" amesema Kimani.

Kimani ameeleza kuwa shule ambazo zitafanya watapewa zawadi ili kutoa hamasha kwa washiriki zaidi.

Msimamizi wa mdahalo Shule ya Al Mutanzir Islamic Gertrude Mtenga, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha shule yake inafanya vizuri.

Amesema kuwa mwaka huu wanafunzi wake watashika nafasi ya kwanza kutokana na elimu ya kutosha waliopewa.

"Mwaka wa jana hatukuweza kushika nafasi ya kwanza ila mwaka huu tutafanya vizuri kutokana wanafunzi wangu wamefanya maandalizi yakutosha" amesema Mtenga.

Amefafanua kuwa mdahalo kwa wanafunzi ni muhimu kwani inamsaidia kuwa katika hali ya kujiamini, kujifunza mambo mbalimbali kwa muda mfupi pamoja na kuwa na uwelewa wa kupanga hoja wakati wa kuzungumza.

Kwa upande wa wanafunzi wamejipanga vizuri katika kuhakikisha kila mtu anafanya vyema katika mashindano hayo.

Mwanafunzi wa Shule ya Al Mutanzir Islamic Husseina Nurbhai, amesema kuwa kutokana na maandalizi waliofanya kabla ya mdahalo huo wanaamini watafanya vizuri.

Nurbhai anasoma kitato cha nne mchapuo wa sayansi, ameeleza kuwa licha ya changamoto baadhi ya mada hasa katika uchumi  atajitaidi ili kuhakikisha Shule yake inakuwa mshindi wa kwanza.

Naye Saloha Aboud amesema kuwa amejipanga kushindana na shule nyingine katika mada mbalimbali ambazo anashiriki katika mdahalo.

"Kwa sasa nina uzoefu wa kutosha katika mashindano hayo kwani niliadha tangu nikiwa kidato cha pili, naamini nitafanya vizuri" amesema Aboud mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya seminari ya Al Mutanziri Isramic.







Hivyo makala AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR.

yaani makala yote AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/al-mu-mustanzir-yawakutanisha-wanafunzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "AL MU MUSTANZIR YAWAKUTANISHA WANAFUNZI AFRICA KWENYE MDAHALO DAR."

Post a Comment

Loading...