Loading...

BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO.

Loading...
BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO.
link : BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO.

soma pia


BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO.


Madiwani pamoja na wakuu wa idara wa Manispaa ya Ilala wakiwa katika kikao cha robo nne ya mwaka katika Baraza na madiwan kilichofanyiika leo jijini Dar es Salaam.

Diwani wa Kata ya Tabata (CHADEMA) Patrick Asenga akichangia mada katika kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela akichangia mada katika kikao cha baraza la Madiwani leo jijini Dar es Salaam.


Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko.
Diwani kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe akisoma taarifa ya Kamati ya Uchumi na huduma za kijamii.

Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala limefanikiwa kukamilisha mipango mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo sekta ya elimu, mazingira katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka.

Wakitoa taarifa za utekelezaji katika kamati mbalimbali kwa nyakati tofauti katika kikao cha Baraza la Madiwani lililofanyika leo jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa Baraza hilo Mstahiki Meya Mhe. Charles Kuyeko.

Kwa upande wa Kamati ya Uchumi na huduma ya jamii Manispaa ya Ilala imefanikiwa kwa kiasi fulani baada ya kufanikiwa kununua pikipiki 30 kwa ajili ya kuwapatia Afisa ya elimu katika kila Kata.

Katika michezo na  UMISSETA na UMITASHUMTA imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kati ya Wilaya zote ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Hata hivyo katika idara ya mipango miji na mazingira kumekuwa na mafanikio kutokana na jitiahada zinaendelea kufanywa na Manispaa ya ilala.

Licha ya mafanikio hayo kumekuwa na changamoto katika kufikia malengo husika.

Akizungumza na kikao cha Baraza Madiwani Manispaa ya Ilala Mstahiki Meya wa ilala  Charles Kuyeko, amesema kuwa kuna changamoto ya mkandarasi katika Kata nne  ambaye anadaiwa anafanya kazi kinyume na makubaliano.

Mhe. Kuyeko ameeleza kuwa mkandarasi huyo ambaye aliomba kufanya kazi bila malipo ya kuhamasisha suala la Usafi katika kata nne ikiwemo Tabata lakini amekuwa na nia ya kuwapiga faina wananchi wanochafua Mazingira bila kuwa na utaratibi maalumu.

"Mkandarasi huyo aliomba kuhamasisha  kufanya usafi bila gharama lakini baadhi ya madiwani katika kata husika wamekuwa na wasiwasi juu ya mkandarasi" amesema Mhe. Kuyeko.

Amesema kuwa  maamuzi ya kumsimamisha mkandarasi huyo wanatarajia kutangaza tenda ili kutoa fursa kwa wengine ili waweze  kufanya kazi hiyo.

"Tuaangia uwezokano wa kusitisha mkataba wake ili kuwapa fursa wengine wafanya kazi" amesema Mstahiki Meya Kuyeko.

Changamoto hiyo imejitokeza baada ya madiwani kutoa taarifa Manispaa kuhusu wasiwasi wao juu ya mkandarasi huyo.

Diwani kata ya Segerea, Edwin Mwakatobe, amesema kuwa kumekuwa na maswali mengi kuhusu mkandarasi huyo.

Amesema kuwa aliomba kazi ya kufanya kazi kwa ajili Kwa kujitolea ya kuelimisha jamii kuhusu utuzaji Mazingira.

"Tulimwambia tuitishe mkutano wa wananchi ili atoe elimu ya mazingira lakini amekataa, eti anataka kupita nyumba hadi nyumba Ndio tulipoingiwa na wasiwasi anataka kuwatoza faini wananchi" amesema Mwakatobe.

Diwani wa Kata ya Tabata Patrick Asenga, amesema lengo ni kuwasaidia wananchi katika mambo mbalimbali kulingana na kile ambacho tunaona inafaa.

"Kwa sasa tumewazuia kufanya shughuli zao ndio maana wamekwenda kwa Mkurugenzi kutoa taarifa ila maamuzi ya Baraza wamekata" amesema Asenga.

Katika hatua nyengine aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela, amewashukuru sana wanafanyakazi wa Manispaa ya Ilala.

Amesema mafanikio aliyopata kwa muda wa miaka miwili imetoka na ushirikiano na Madiwani wote katika kuleta maendeleo.

Palela amewataka Madiwani wote kuendelea kutoa ushirikiano katika Manispaa ya ilala ili kuhakikisha wanaendelea kupiga hatua za kimaendeleo.













Hivyo makala BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO.

yaani makala yote BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/baraza-la-madiwani-ilala-yafanikisha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "BARAZA LA MADIWANI ILALA YAFANIKISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO."

Post a Comment

Loading...