Loading...
title : Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini
link : Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini
Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini
Naibu waziri wa madini, Dotto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa eneo la Kilalani, baada ya kutembelea eneo hilo.
Na Zuena Msuya, Tanga
Serikali imempa muda wa wiki moja nwekezaji mmiliki wa kampuni ya Amazon Trading (T)Company Limited Abdi Hozza kuhakikisha anailipa serikali kodi ya pango ya uwekezaji kiasi cha dola za Marekani 70,020 sawa na zaidi ya shilingi milioni 140 za kitanzania anazodaiwa tangu mwaka 2011 katika machimbo ya Kalalani eneo la Umba wilayani Korogwe kutokana na leseni nane za uchimbaji wa madini kuanzialeseni namba (102-109/2001) anazomiliki .
Sambamba na hilo imeiagiza serikali ya wilaya ya Korogwe kuhakikisha inatenga maeneo ya wachimbaji wadogowadogo wa madini ili kuepusha migogoro iliyodumu kwa muda mrefu hali ambayo imeleta hali ya chuki baina ya mwekezaji na wananchi.
Waziri Biteko alitoa agizo hilo alipotembelea katika machimbo hayo juzi Jumamosi katika vijiji vya Kigwasi na Kalalani kata ya Kalalani wilayani humo. Biteko alimtaka ndani ya wiki moja mwekezaji huyo kulipa kodi hiyo ya pango anayodaiwa na serikali na amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuwabaini wageni na watu wanaonunua madini kwa njia za panya.
Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko, akikagua Mabaki ya mgodi wa Amazon,ambao umesitisha uchimbaji kwa miaka mingi kutokana na Matatizo mbalimbali.
“Haiwezekani tangu madini yaanze kuchimbwa katika machimbo haya serikali haijapata kodi kutokana na mgodi huu tunakuta sifuri nimewaambia wailipe haraka nataka nikifika Dodoma kuna commitment statement mnalipa lini” alisema.
Aliongeza “Na yule anayedhani atakuja Kalalani kununua madini kwa njia ya panya muda huo umekwisha,na tumekwenda kwenye mto tumekuta mnachimba madini,sheria inakataza kuchimba madini kwenye vyanzo vya maji naomba kuanzia sasa mkaondoe vifaa vyenu kule mtoni”.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini
yaani makala yote Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/biteko-atoa-wiki-moja-kwa-muwekezaji.html
0 Response to "Biteko atoa wiki moja kwa muwekezaji kulipa kodi ya madini serikalini"
Post a Comment