Loading...
title : CCM Wilaya ya Ilala watoa agizo Kamati ya utekelezaji UWT Wilaya
link : CCM Wilaya ya Ilala watoa agizo Kamati ya utekelezaji UWT Wilaya
CCM Wilaya ya Ilala watoa agizo Kamati ya utekelezaji UWT Wilaya
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja wa Wanawake UWT wakiwa katika kikao cha baraza Dar es salaam Jana (PICHA NA HERI SHAABN)
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT wilaya ya Ilala BATULI MZIYA akisalimiana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga Mwita waitara katika kikao cha Baraza la UWT Dar es salaam Jana (Picha na HerI Shaaban)
Na Heri Shaban
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Ubaya Chuma ametoa agizo kwa Katibu wa Umoja wa Wanawake wa wilaya ya Ilala UWT kuwachukulia hatua Kali viongozi wa Kamati ya Utekelezaji UWT ambao wanashindwa kushiriki vikao vya jumuiya .
Akitoa agizo hilo katika Baraza la UWT Wilaya ya Ilala Dar es salaam Jana ambalo pia baraza hilo lilitumia nafasi hiyo kutamburishwa Mgombea Ubunge wa Ukonga tiketi ya CCM Mwita Waitara.
"Katibu wa UWT Winne Mtaki, nakuagiza kuanzia Leo naomba wote ambao Wapo katika Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Kamati ya utekekezaji na Leo hawakufika katika Kikao chako cha Baraza walete taarifa zao kwa maandishi "alisema Ubaya Chuma.
Chuma alisema kila mtu aliomba nafasi jumuiya na chama wakati anaomba alisema anaweza hivyo kila mtu atekeleze majukumu yake na kusimamia misingi ya chama na kufanya kazi zake kwa weledi bila kuvuka mipaka.
Alisema chama cha mapinduzi CCM inategemea jumuiya zote mbili za UWT na UVCCM kwa uhai wa chama hivyo mda wote ziwe imara na kila mtu kusimamia majukumu yake.
"Wakati mnaomba hizi nafasi tumeacha watu Wazuri wengi pia wanauwezo kwa nini nyie ambao mmechaguliwa mnashindwa kutekeleza wajibu wenu "alisema.
Wakati huohuo alisema Hali ya kisiasa kwa sasa Wilaya ya Ilala safi baada muda tutapata Meya wa jiji la Dar es salaam kutoka CCM pia hata Meya wa Ilala hivyo baadhi ya Kata zikae mkao wa uchaguzi madiwani wa Ilala wameonyesha mapenzi mema na CCM na utekekelezaji wa ILANI ya chama cha mapinduzi unaofanyawa na Rais wa awamu ya tano John Magufuli.
Kwa upande wake KATIBU wa Umoja wa Wanawake UWT wilaya ya Ilala Winne Mtaki,akitoa taarifa ya miezi sita alisema wilaya ya Ilala ina wakazi 1,220,611 Kati yake Wanawake 624683 wanaume 59,928 na Kata 36 na mabarozi wa mashina Wanawake 678.
Winne alisema UWT Wiilaya ya Ilala Mpango kazi wake wamejiwekea kuingiza wanachama wengi zaidi moja ya mkakati tuliojiwekea katika kuongeza wanachama kila siku kuanzia miaka 18 hadi 35.
Aidha pia alisema jumuiya hiyo inatarajia kufanya semina elekezi ya viongozi ili kuimalisha uongozi ndani ya jumuiya yetu kwa kupita kila Kata na matawi.
Dhumuni lake kuimalisha uhai wa jumuiya sambamba na uhakiki wa wanachama, kutembelea vikundi mbalimbali kusikiliza kero pamoja na uandaaji wa semina za Wajasiliamali Wanawake.
Akizungumzia mafanikio UWT Wilaya ya Ilala imefanikiwa kupata wanachama wapya wa UWT 13788 kutoka wa zamani 31482 .
Pia wamefanikiwa kuwamasisha Wanawake kugombea nafasi mbalimbali za JUKWAA La Wanawake ili waweze kujiinua kiuchumi.
'"UWT Wilaya ya Ilala kwa sasa ipo vizuri tumefanya mengi mazuri ikiwemo kupeleka viongozi wa Kata na wanachama katika semina ya ujasiriamali ambayo ilifanyika Jimbo la Ukonga na walipewa vyeti vya mafunzo "alisema
Hivyo makala CCM Wilaya ya Ilala watoa agizo Kamati ya utekelezaji UWT Wilaya
yaani makala yote CCM Wilaya ya Ilala watoa agizo Kamati ya utekelezaji UWT Wilaya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CCM Wilaya ya Ilala watoa agizo Kamati ya utekelezaji UWT Wilaya mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/ccm-wilaya-ya-ilala-watoa-agizo-kamati.html
0 Response to "CCM Wilaya ya Ilala watoa agizo Kamati ya utekelezaji UWT Wilaya"
Post a Comment