Loading...
title : CWT WILAYANI NAMTUMBO WAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WAO
link : CWT WILAYANI NAMTUMBO WAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WAO
CWT WILAYANI NAMTUMBO WAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WAO
DC Mfaume awaahidi makubwa, awapongeza
CHAMA cha Walimu Tanzania(CWT) wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wamekumbushwa kwamba chama hicho ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya walimu.
Wameambiwa hicho si chama cha kiuanaharakati wala chama cha siasa na kwamba wajikite kwenye lengo lao la msingi. Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume amewaambia viongozi wa chama hicho leo kuwa Serikali inatambua changamoto zinazowakabili walimu zikiwemo upandaji wa madaraja na madai mengine.
Amewatoa wasiwasi kwamba madai yao yanashughulikiwa huku akiahidi kuendelea kuboresha mazingira yao ya kazi ikijumuisha na miundombinu Pia Mfaume amewakumbusha CWT kwamba katika moja ya ziara alizofanya, wazazi walilalamika kuhusu adhabu kali zinazotolewa kwa wanafunzi shuleni. " Mfano adhabu ya kuwafyatulisha wanafunzi matofali 1000 wanapofanya makosa.
Hivyo nituwaombe walimu kutumia busara adhabu wanazotoa mashuleni... "Kwani wasipotumia busara tatizo la utoro kwa wanafunzi litaongezeka," amesema Mfaume huku akiwapongeza kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya. Ameongeza na hasa ikizingatiwa kwamba ufaulu wa wanafunzi hasa wa sekondari ni wa kuridhisha.
Mfaume amewaahidi CWT ushirikiano wa kutosha na kuwasihi waendelee kuchapa kazi. Mkuu wa Wilaya huyo amekuwa akitumia muda msingi akifanya ziara ya kutembelea na kukagua maeneo mbalimbali. Ambapo lengo lake kubwa ni kuhakikisha anasikiliza kero za wananchi wa Namtumbo na kisha kuzipatia ufumbuzi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa Wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Mfaume (tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma,mara baada ya kuzungumza nao
Baadhi ya Waalimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh Sophia Mfaume (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wilayani humo kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo na kuelezwa kuwa cha hicho si kiuanaharakati wala si chama cha siasa na kwamba wajikite kwenye lengo lao la msingi.
Hivyo makala CWT WILAYANI NAMTUMBO WAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WAO
yaani makala yote CWT WILAYANI NAMTUMBO WAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CWT WILAYANI NAMTUMBO WAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/08/cwt-wilayani-namtumbo-wakumbushwa.html
0 Response to "CWT WILAYANI NAMTUMBO WAKUMBUSHWA KUZINGATIA WAJIBU WAO"
Post a Comment